Habari za Punde

MTOTO AANGUKA MICHENZANI, AFARIKI

Na Halima Abdalla

NADIL Muhammed Mselem (5) mkaazi wa Mpendae amefariki dunia baada ya kuanguka kutoka kwenye jumba namba 7 la Michenzani ngazi ya pili ghorofa ya tano wakati akicheza.


Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Aziz Juma Mohammed alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 4:00 asubuhi wakati mtoto huyo alipokwenda kwa jamaa zake kuwatembelea kipindi hicho cha sikukuu.

Kamanda alisema marehemu alifikishwa katika hospitali ya Mnazimmoja na amezikwa kwao Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja.

Kamanda alitoa wito kwa wazazi kuwa waangalifu na watoto wao wanapocheza katika maeneo mbali mbali yenye hatari ili kuepusha matatizo kama hayo.

Wakati huo huo Mwashungi Muhene Hamad (33) mkaazi wa Sokomuhogo alipatikana na kete za unga 12 zinazosadikiwa kuwa ni dawa za kulevya huko Malindi mjini hapa

1 comment:

  1. Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu na awape subra wazazi wake. Ama hao kina mwashungi tena waliokusudia kutuharibia nchi vyombo vya dola vifanye kazi yake!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.