Habari za Punde

RAMBI RAMBI KUTOKA ZANZIBAR FOR DEMOCRACY (UK)

Viongozi na wanachama wa Zanzibar For Democracy(UK) tumezipokea habari za kuzama kwa meli ya Spice Islands kwa huzuni, masikitiko na unyonge sana.Aidha, tumepata maumivu sana kwa vifo vya wananchi wengi ambao walikuwemo katika meli hiyo.


Tunaomba kuchukua nafasi hii ili kutoa salamu zetu za pole kwa familia, ndugu na jamaa wa marehemu waliopoteza maisha yao katika ajali hiyo.Vile vile tunaiomba serikali kuchukua hatua zifuatazo ili kunusuru maisha ya wananchi wanaosafiri kwa kutumia vyombo vya baharini.

(a)Kuhakikisha kuwa vyombo vyote vya baharini vinavyosafirisha abiria vinakaguliwa kwa kutumia viwango vya kimataifa;
(b)Vyombo hivyo vinapakia idadi halisi iliyokubaliwa kisheria;
(c)Vyombo vyote vilivyochakaa visiruhusiwe kuingizwa nchini na vile vilivyopo visiruhusiwe kusafiri;
(d)Serikali ichukue juhudi za makusudi za kuwapatia wananchi vyombo vya kisasa katika vivuko vyote vyenye kutumiwa na wananchi wengi, isiwache jukumu hili mikononi mwa watu binafsi;
(e)Serikali ifanye uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo, na mapendekezo yatakayotolewa yafanyiwe kazi kwa lengo la kuimarisha na kudumisha usafiri wa uhakika na usalama kwa wananchi.

Tunaungana na wananchi wote katika kuomboleza msiba huu mkubwa uliotokea.
Inshallah Mwenyezi Mungu awape wafiwa wote subira, stahmala uvumilivu kwa msiba huo na awalaze marehemu wote peponi(Amin).

Ahsante,

Abdulla A. Abdulla,
Katibu,

Zanzibar For Democracy(UK)

(07853180339)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.