Habari za Punde

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUTOKA ZANZIBAR COMMITTEE FOR DEMOCRACY - DENMARK

Mheshimiwas Rais Shein, 12 September, 2011

Kwa wingi wa huzuni na mastaajabu,tumepokea habari ya kuzama kwa meli ya `Spice Islanders`. Vile vile, isije ikafahamika na kuchukuliwa kua akina sisi ni watu wasiofahamika,kwa kutoweza kutoa pole zetu na huzuni kwa idadi ya hao ndugu zetu waliopateza maisha yao. Hasa vile tunavyotambua kwamba, kila roho moja ya Binadamu tumetunukiwa na mwenyewe Mola. Kwa wakati mgumu kama huuu, hatuna budi kutoa salamu za majonzi kwa Viongozi wetu pamoja na wafiwa wote. Mungu awalaze mahali pema Amin.

Mastaajabu yetu makubwa yapo pale tunapotia shaka kubwa kwa yanayo tangazwa kwamba,ulipitikana uzembe, nao sio kwa mara ya kwanza, kwa wale wenye dhamana ya utendaji kutokuwa na nia au uwezo wakutekeleza majukumu waliyopewa. Hii ni shutuma nzito. Kwa hivyo,uzito wa jambo hili, unauwajibisha Serikali yetu kuunda tume huru, yenye mamlaka mapana kuchunguza sababu iliyopelekea meli kuzama, ili kitendo kama hichi kisiweze kutokea tena kwa siku zijazo .

Tumevutiwa sana namna serikali pamoja na Wananchi walivyojitolea kwa kuwanusuru waliozama. Hili ni janga la Kitaifa. Bila shaka msaada wa dharura unahitajika kwa walio salia.

Hatutosahau vile vile kushukuru (blog ya Jikumbuke), kwa kazi nzuri na ya kupigiwa mfano, kwa waliyoyafanya kuweza kusambaza kwa wengine kuweza kujua yaliyotokea.

Kwa niaba:
Hashil Seif Hashil
Zanzibar Committee
For Democracy
Gustav Bangs Gade 11st, th
2450 Copenhagen SV
Denmark.
+45 22726491

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.