Habari za Punde

KUTOKA BARAZANI - SERIKALI YAKIRI UTENDAJI SHIRIKA LA MELI SI WA KURIDHISHA

SERIKALI ya Zanzibari imesema kwamba Utendaji wa Shirika la Meli Zanzibar hivi sasa sio mzuri kutokana na meli zake kuchakaa kiasi ambacho linakosa ufanisi katika utoaji wa huduma zake kwa wananchi.

Naibu Waziri wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Issa Haji Gavu, alieleza hayo barazani jana wakati akijibu suali la Mwakilishi wa Mtambwe, Rashid Seif alietaka kujua ni kwanini serikali imekuwa ikiliita shirika la Meli huku taasisi hiyo ikiwa haina meli hata moja.


Akijibu hoja hiyo Naibu Waziri huyo alisema ni kweli shirika hilo hivi sasa linakabiliwa na hali hiyo kutokana na kuchakaa kwa meli zake lakini tayari serikali inajiandaa kutafuta njia za kukabiliana nalo.

Akijibu suali la Mwakilishi wa Mtambwe, Salim Abdalla Hamad aliehoji kama Shirika la Bandari lina mpango wa kurefusha Chelezo chake ili kiweze kuzihudumia meli kubwa ambazo zinahitaji kufanyiwa matengenezo hapa nchini.

Akijibu, alisema ingawa Shirika hilo limeruhusiwa kufanya biashara lakini linakabiliwa na mahitaji makubwa na yenye kuhitaji fedha nyingi.

Kutokana na hali hiyo Naibu huyo alisema haitakuwa jambo la busara kwa serikali kulipatia shirika hilo meli ambazo zipo chini ya usimamizi wa Shirika la Meli.

Hata hivyo, Naibu huyo alisema kutokana na kuwepo uwiano wa utendaji wa shughuli za taasisi hizo shirika hilo linaweza kufikiria kufanya biashara ikiwa litakuwa na fedha ya kufanya hivyo.

Alisema hivi sasa Shirika la Bandari linashindwa kutekeleza hilo kutokana ka tatizo la ukosefu wa fedha na inachokifanya hivi sasa ni kuwekeza zaidi katika ununuzi wa vifaa vya kushughulikia mizigo ingiapo nchini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.