Habari za Punde

MBUNGE NA MWAKILISHI WA JIMBO LA RAHALEO ZANZIBAR WATOWA MCHANGO WAO.JIMBONI.

MBUNGE NA MWAKILISHI wa Jimbo la Rahaleo Abdalla Juma na Nassor Salim Jazira, wakimkabidhi Pump ya Kisima Shekha wa Shehia Mwembeshauri Bakari Othman, kwa ajili ya kisima cha chao baada ya kuharibika ya zamani na kukabidhiwa hiyo mpya kwa matumizi ya jimbo hilo shehia ya Mwembeshauri. 

 Mbunge wa Rahaleo akimkabidhi Charahani Mwenyekiti wa Vijana Tawi la Muembeladu Azizi Yussuf kwa ajili ya Kikundi cha Vijana wa Kike waliopata mafunzo ushoni na kukabidhiwa vitendea kazi na  Mbunge na Mwakilishi katika ukumbi wa Klabu ya Ujamaa.
 MBUNGE wa jimbo la Rahaleo Dk.Abdalla Juma akitowa nasaha zake kwa Vijana wa Vikundi vya Wanawake katika sherehe za kuwakabidhi vitendea kazi za ushoni vijana hao baada ya kupata mafunzo kwa ajili ya kuazisha vikundi vya Ujasiriamali jimboni.
 MWAKILISHI wa Jimbo la Rahaleo Nassor Salim Jizira akiwapongeza Vijana wa Kike wa jimbo hilo kwa kufuzu mafunzo yao ya Ushoni katika sherehe za kukabidhi vitendea kazi vyao.
 KATIBU wa Wazazi jimbo la Rahaleo Mwanabaraka Khamis Shehe akimkabidhi mbunge risiti za vijana waliomaliza mafunzo yao ya ushoni na kukabidhiwa vitendea kazi vya ushoni charahani nne kwa ajili ya kikundi chao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.