WAZIRI wa Afya Zanzibar, Juma Duni Haji (kushoto) akitia saini makubalianao ya ujenzi wa hospitali za kisasa zitakazojengwa Zanzibar na jumuiya ya Mwezi Mwekundu ya Iran, makubaliano hayo yalitiwa saini mjini Dubai Falme za Kiarabu. Katikati waliosimama ni Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad pamoja na maafisa wa jumuiya hiyo. (Picha na Salmin Said, OMKR).
. Moja kujengwa Wete nyengine Mjini Magharibi
. Maalim Seif ashuhudia utiaji saini Dubai
Na Khamia Haji, OMKR
JUHUDI za serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuinua huduma za afya kwa wananchi, ikiwemo kuwapunguzia gharama za kwenda kutibiwa nje ya nchi zimeanza kuonesha dalili za mafanikio baada ya serikali kutiliana saini makubaliano ya ujenzi wa hospitali mbili za kisasa zitakazojengwa katika mji wa Wete Pemba na mkoa wa Mjini Mgharibi Unguja.
Hospitali hizo zitajengwa na Jumuiya ya Mwezi Mwekundu ya Iran (Iran Red Crescent Society) mara baada jumuiya hiyo kukamilisha utafiti wa mahitaji ya afya ya wananchi wa Zanzibar unaotarajiwa kukamilika mwezi Disemba mwaka huu.
Hatua hiyo inafikiwa baada ya serikali ya Zanzibar kutiliana saini makubaliano ya mradi huo huko Dubai, Falme za Kiarabu wiki iliyopita, ambapo Waziri Afya na Ustawi wa Jamii, Juma Duni Haji alitia saini hiyo kwa niaba ya Zanzibar, huku Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad akishuhudia tukio la utiaji saini makubaliano hayo.
Waziri wa Afya, Juma Duni amesema chini ya makubaliano hayo, jumuiya hiyo itajenga hospitali za kisasa zitakazotoa mahitaji yote, ambapo Zanzibar jukumu lake itakuwa ni kuipatia sehemu zitakazojengwa hospitali hizo katika mkoa wa Mjini Magharibi na huko Wete kwa upande wa Pemba.
"Serikali ya Zanzibar haitatoa fedha yoyote katika ujenzi huo, isipokuwa maeneo yatakayojengwa hospitali hizo, baada ya hatua ile ya utiaji saini watafanya utafiti wa mahitaji halisi ya kiafya ya Wazanzibari ambao utakuwa umekamilika ifikapo mwezi Disemba mwaka huu na ujenzi utaanza", alisema Waziri Duni.
Alieleza kuwa utafiti huo pia utajumuisha mahitaji ya uajiri kwa madakatari watakaohitajika katika hospitali hizo, pamoja na taratibu za kuwapatia vibali vya kufanyia kazi kwa madaktari wageni watakaohitajika kuja kuhudumia wagonjwa.
Duni alisema jumuiya hiyo ya Mwezi Mwekundu ya Iran ni ya hisani (Charitable Society) ambayo tayari imejenga miradi mikubwa ya hospitali katika miji mbali mbali, ikiwemo Dubai na huduma inazozitoa zimesifiwa juu ya ubora wake na hata unafuu katika upatikanaji wake kwa wananchi wenye vipato vya chini.
Alieleza kuwa walipokuwa Dubai walitembelea moja ya hospitali zinazoendeshwa na jumuiya hiyo, ambayo inatoa huduma zote muhimu katika kiwango cha hali ya juu na wagonjwa wengi wamekuwa wakienda kupata huduma kwa unafuu.
Waziri Duni alisema hospitali hizo zitakapoanza kutoa huduma Zanzibar itakuwa ni hatua kubwa na ya mafaniko kwa wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba kupata matibabu, kwa sababu hadi sasa huduma zinazopatikana nchini hazijatosheleza na kuna wananchi wengi wanaopewa rufaa kwenda kutubiwa nje ya nchi, jambo ambalo sio wananchi wote wanaoweza kumudu gharama zake.
Alisema faraja kubwa zaidi itakuwa kwa wananchi wa kisiwa cha Pemba, ambao hata kesi ndogo za matibabu mara kadhaa hutakiwa kuja Unguja katika hospitali ya Mnazimmoja, jambo ambalo pia alisema ni mzigo kwao kutokana na hali za kimaisha za wananchi wengi bado ni duni.
"Hospitli itakayojengwa Wete kule Pemba ina umuhimu mkubwa zaidi ikizingatiwa kwamba, hata kesi za kawaida wao hutakiwa kuja Unguja na kutumia gharama nyingi za usafiri na matibabu yenyewe", alisema.
Ijumaa iliyopita, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema serikali inachakua juhudi kubwa kuhakikisha huduma za kisasa na za kiwango cha juu za matibabu zinapatikana Zanzibar kwa nia ya kuwaondolea usumbufu na gharama kubwa wanazopata wananchi pamoja na serikali, pale wanapotakiwa kwenda kufanyiwa matibabu zaidi nchi za nje.
Akizungumza na madaktari kutoka hospitali ya MIOT ya India walipomtembelea ofisini kwake, alisema bado Zanzibar inahitaji wataalamu waliobobea zaidi katika sekta mbali mbali, ikiwemo ya afya kufanikisha azma ya kuwapatia wananchi wa Unguja na Pemba huduma za matibabu za uhakika na kwa urahisi.
Maalim Seif alisema hadi sasa kesi za wagonjwa wanaotakiwa kupatiwa matibabu ni nyingi, ikiwemo watoto wadogo wanaosumbuliwa na maradhi ya moyo, ambao hutakiwa kwenda kufanyiwa upasuaji nchini India wakifuatana na jamaa pamoja na mhuduma wa afya, ambapo serikali na wananchi watapata nafuu kubwa iwapo huduma kama hizo zitakapokuwa zinapatikana hapa hapa Zanzibar.
Mbali na nchi za nje baadhi ya wagonjwa hapa Zanzibar hutakiwa kwenda kupata matibabu zaidi katika hospitali za Tanzania Bara, pale huduma husika zinapokosekana katika hospitali za Zanzibar.
Sasa ndio SMZ itaziona gharama za kushindwa kusimamia ardhi vizuri!..Tutaona wapi watatoa kiwanja cha kujenga hospitali kubwa na kisasa kama hiyo, na bado EAC ina mpango wa kujenga chuo kikuu cha kiswahili na utamaduni..sijui itakuwaje? Maeneo ya wazi yameshajengwa, serikali imeshindwa kupima viwanja,ikajulikana vipi ni vya makaazi na vipi ni vya serikali.kubwa zaidi kule mazizini na chukwani kumeshajaa,Tunguu nako hoi,heka nazo hazisimamiwi, waliopewa wanaziuza na kuzijenga ovyo ovyo.Blozi Seif peke yake atafanya lipi aache lipi..tatizo letu kubwa ni uvivu wa kufikiri. Labda watoe tu yale majengo yaliyotelakezwa pale pembeni ya mnazi mmmoja na nna hakika hayatoshi!
ReplyDeleteMie nahisi iko haja ya kujadili motives za serikali ya Iran kusaidia ujenzi wa hospitali hizi. Ukiliangalia juujuu hili suala utaona kuwa hawa ni jamaa wameona kuwa sisi tuna shida ya hospitali na wameonelea kuwa watusaidie. Lakini wanasiasa hawafanyikazi namna hiyo. Lazima huwa wana interests zao. Sasa hawa Wairan wanataka kitu gani in return baada ya kutoa msaada kama huu.Huenda hili likawa ni suala ambalo litakuja kutugonganisha vichwa baadae. Anyway, ndio matatizo ya maskini. Ukipewa unaogopa kukataa. Lakini nahisi hapa lipo neno. Mungu atasaidia.
ReplyDeleteIkiwa makaffir (maadui zetu na maadui wa M/Mungu)na ambao walitutawala, hatuhoji misaada yao pale wanapotusaidia iweje kwa ndugu zetu ktk imani? Tuachane na fitna za magharibi ambao wamewafitinisha ndugu zetu pale mashariki ya kati wote hawaelewani! na sisi tusije tukaingia ktk mtego huu. Hebu tijiulize.. hivi kweli Iran itakua adui kwa waarabu na waislamu wa sunni kuliko wayahudi na manaswara? Tumechoshwa na mawazo ya 'waarabu'! hatutaki tena kugawanywa!..Mara..shia,mara sunni,mara Ismailiyya mara Ahmadia,mara Bohora mara Ithnashir mara Alawitt, mara suffy.Ukija hapa kwetu ndio ..oho mara ahal-tariq mara mwezi wa makungu mara wa saudia. Tofauti hatuwezi kuzizuia na aliye tamka La ilaha- illa- llah ni bora kuliko wengine ..hebu tufanye hizi ni tofauti zetu za ndani..makafiri wasituchezee!
ReplyDeleteMimi nahisi kuna haja ya kujadili what is the motive na sio kurukia ushia, uarabu na sunni kitu ambacho hakikutajwa mahali popote. Kuna nia gani ya hawa Wairani kutaka kusaidia Zanzibar? Hawa jamaa hivi majuzi tu wamepatikana na njama za kutaka kumuuwa balozi wa Saudia nchini Marekani. Hapa kuna neno naomba wachambuzi watusaidie.
ReplyDeleteSasa kaka si unarudi pale pale nliposema makaffir wanatufitinisha, kuna ushahidi gani ktk hilo? Tukiamua kuamini fitna, tuamini tuu! ..kuna tuhuma pia kwamba wanatengeneza silaha za nyuklia,hivi kweli taifa la kiislamu halipaswi kumiliki nyuklia? Pili wanatuhumiwa kuisaidia Hizbu-llah na Hamas ktk vita vyao dhidi ya Israel hivi kweli Wayahudi wana haki ya kuwaonea wapalestina na kuichukua Jerusalem ya mashariki?
ReplyDeleteUshahidi wa kuwepo njama za kutaka kumuuwa balozi wa Saudia Marekani ni pamoja na wire transfers(pesa kutoka benki) ya Iran zinazofikia dola laki mbili ambazo aliletewa huyu mtu ambae alikuwa na huo mpango wa kuua. Pia amerekodiwa kwa maneno yake mwenyewe na tape zipo kama ushahidi kuwa ana mpango huo wa kuuwa sasa sijui unataka ushahidi gani.
ReplyDeleteKuhusu ukafiri wa Marekani hilo mimi sipingi hata kidogo na urafiki wao na Israel ambao wanawauwa wapelestina(Lakini serikali ya Tanzania na Zanzibar pia wana uhusiano na Israeil).
Nnachokiuliza mie ni jee hawa Wairan wana nini wanachokitaka kwa Wazanzibari. Historia inaonesha kwamba hakuna msaada wa bure. KUNA NINI HAPA?
Mwaka 2005 nilikutana na mmoja wa Wakuu katika Wizara ya Elimu ambaye alinijuulisha kwamba Wairan walikujana mpango wa kutaka kuanzisha Chuo Kikuu Zanzibar cha Engineering and Technology.
ReplyDeleteKwa maoni yangu pia niliwatahadharisha ujio wao kupitia mgongo wa Chuo. Sijui project hii ilimalizikia vipi maana sikupata update zake.
Waswahili tumeshaimba Ina hatari misaada ...
Hii ndio shida ya kuwa 'brain washed' kuamini kwamba kila wanachosema west ndio sahihi!Ushahidi unaoutoa kaka ni tuhuma(suspecion) zilizotolewa na vyombo vya habari vya magharibi na ambazo bado ni 'premature' zinahitaji kuthibitihwa na vyombo huru na sio US pekee! Hayo maelezo hata mimi niliyaona juzi ktk BBC lkn siku hizi najaribu kuacha 'ukasuku' na kufikiri 'other wise' saudia yenyewe ili react kwa kusema 'kama ikithibitika,basi Iran italipa gharama' iweje kaka sisi tu jump into conclusion?Tukumbuke UK. walisema Iraq ina silaha za maangamizi, leo hii wadai 'was unfortunate' waliokubali ukasuku wao hawajui wasemeje! Ni kweli Tza tuna uhusiano na Israel lkn hatuungi mkono kila wanachofanya! Ndugu yangu tukiamua kuhoji misaada tuhoji yote sio ya Iran pekee! wenzetu bara wamesaidiwa power tiller(tractors)100 hakuna aliyehoji.Mimi naamini Iran hawana lolote la kutufanya zaidi ya kueneza 'ushia'ambao sio issue na kutaka kuungwa mkono UN kwenye makasheshe yao ya nyuklia kama ikipigwa kura! Na ndugu yangu kama ulichangia kwa njia yeyote ile kuzuia project ya ujezi wa hicho chuo cha ufundi kwa kweli hukututendea haki wazanzibari na utuombe radhi!..Mwisho nadhani 'tutangaze interest' isije ikawa tuna bishania issue ya kiimani?..maana hatuta pata suluhisho!
ReplyDelete