JUMUIYA za Wafanyabiashara na Wenyeviwanda za Sharjah na Ras Al Khaimah zimeahidi kushirikiana na Zanzibar katika kuimarisha sekta za biashara, viwanda na uwekezaji pamoja na kuanzisha uhusiano wa kutembeleana kati ya Jumuiya hizo na Jumuiya ya Wafanyabiashara, Wenyeviwanda na Wakulima ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein alielezwa hayo na viongozi wa Jumuiya hizo kwa nyakati tofauti wakati wa ziara yake huko Falme za Kiarabu.
Uongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na Wenyeviwanda wa Ras Al Khaimah ulimueleza Rais Dk. Shein kuwa Jumuiya yao imeweza kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya uchumi wa Ras Al Khamah.
Ulieleza kuwa Jumuiya hiyo ambayo imekuwa ikizishirikisha sekta binafsi ipasavyo imepata mafanikio makubwa na iko tayari kuimarisha ushirikiano na Jumuiya ya Wafanyabiashara, Wenyeviwanda na Wakulima ya Zanzibar kwa lengo la kupaa aankio zaidi kwapande zote mbili.
Uongozi wa Jumuiya hiyo ulieleza kuwa tangu Ras-Al-Khaimah ijiunge na Falme za Kiarabu (UAE) imepata mafanikio makubwa katika sekta za biashara, viwanda, uwekezaji na hata utalii kwa kiasi fulani.
Kutokana na hatua hiyo uongozi wa Jumuiya hiyo ulieleza lengo lao la kufanya ziara kwa ajili ya kuitembelea Jumuiya ya Wafanyabiashara,Wenyeviwanda na Wakulima ya Zanzibar na kuangalia maeneo ya kushirikiana.
Dk. Shein aliwakaribisha Zanzibar Wafanyabiashara na Wenyeviwanda wa Ras-Al Khaimah kwa lengo la kushirikiana na wenzao wa Zanzibar katika kuimarisha sekta hizo za kiuchumi.
Nayo Jumuiya ya Wafanyabiashara na Wenyeviwanda ya Sharjah ilieleza haja kwa Jumuiya ya Wafanyabiashara, Weyeviwanda na Wakulima ya Zanzibar kushirikiana pamoja kwa lengo la kuleta mabadiliko na maendeleo ya kibiashara.
Uongozi huo pia, ulieleza kuwa Chuo chake cha Ufundi kimekuwa kikitoa mafunzo mbali mbali yakiwemo mafunzo ya Amali na kueleza kuwa kinawakaribisha Wazanzibari kwenda kupata mafunzo chini ya ufadhil wao.
Pamoja na hayo walieleza kuwa kutokana na kufanyabiashara na kuuza biadhaa zao kwa bei nafuu Sharjah imekuwa ni kivutio kwa wafanyabiashara na wawekezaji wengi duniani na hivyo kueleza haja ya wafayabiashara wa Zanzibar nao kwenda huko.
Dk. Ali Shein katika maelezo yake na viongozi wa Jumiya hizo aliokutana nao kwa nyakati tofauti, alisema kuwa Zanzibar ina mazingira na Sera nzuri ilizoziweka katika sekta za biashara na uwekezaji ambazo zimekuwa zikiishirikisha sekta binafisi kwa lengo la kutoa fursa nzuri kwa biashara na uwekezaji.
Aidha, Dk. Shein alieleza kuwa Zanzibar iko tayari kutuma ujumbe wake huko Falme za Kiarabu kwa lengo la kutoa taaluma juu ya vivutio, fursa na maeneo makuu ya uwekezaji yaliopo Zanzibar.
Katika maelezo yake Dk Shein hakuacha kusisitiza mafaikionyaliopatikana Zanzibar kutokana na amani na utulivu uliopo pamoja na ukarimu wa wananchi wake ambavyo vitu vyote kwa pamoja vina umuhimu mkubwa katika sekta zote za maendeleo ikiwemo uwekezaji na biashara.
Aidha, Dk. Shein alieleza haja ya kuimarishwa kwa mawasiliano kwa njia ya anga na bahari kwa lengo la kukuza na kuendeleza biashara na uwekezaji.
Dk. Shein katika ziara yake hiyo akiwa Sharjah alitembelea Kiwanda cha dawa na kuzungumza na uongozi wa kwanda hicho na kuwaeleza haja ya kuangalia uwezekano wa kupanua soko lake na kufikisha bidhaa zao hadi Zanzibar sanjari na kuangalia uwezekano wa kujenga kiwanda cha dawa Zanzibar.
Alieleza kuwa hatua hiyo itasaidia kuimarisha zaidi soko la bidhaa za kiwanda hicho kwa nchi za Afrika Masharaiki pamoja na nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Bara la Afrika (SADC).
Pamoja na hayo, Dk. Shein alipata fursa ya kutembelea kiwanda cha vifaa vya ujenzi wa nyumba (RAK Ceramics), huko Ras Al Khaimah na kuueleza uongozi wa kiwanda hicho kutafuta uwezekano wa kuanishwa kiwanda kama hicho Zanzibar na kuelezwa kuwa hatua hiyoitafanyiwa kazi na uongozi.
Pia, katika mazungumzo hayo ilielezwa haja kwa wafanyabiashara wa Zazibar kutembelea kiwanda hicho na kuoa bdhaa zinazozalishwa.
Katika ziara yake hiyo Dk. Shein alitoa pongezi kwa wenyeji wake wote kuotkana na mapokezi mazuri aliyoyapata yeye na ujumbe aliofutana nao.
Dk. Shein alitoa salamu za pongezi maalum kutoka kwa wananchi wa Zanzibar kwa ndugu zao wa nchi za Falme za Kiarabu na kueleza kuwa Zanzibar inathamini uhusano na ushirikiano uliopo wa muda mefu ambao utaendelezwa kwa manufaa ya pande zote mbili.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Shein anatarajiwa kurejea nyumbani kesho jioni.
Rajab Mkasaba,UAE
No comments:
Post a Comment