Habari za Punde

PICHA ZA MCHEZO KATI YA ZANZIBAR HEROES NA BURUNDI

MCHEZAJI wa timu ya Taifa ya Zanzibar Suleiman Kassim akimtoka mchezaji wa Burundi Amissi Cedric katika pambano lao la kuwania kombe la Tusker Challenge lililochezwa jana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Pambano hilo lilimalizika kwa sare ya 0 - 0.
MSHAMBULIAJI wa timu ya Taifa ya Zanzibar Ali Badru akiondoka na mpira huku akikabwa na mlinzi wa timu ya Burundi Kaze Gilbert katika pambano la kuwania kombe la Tusker Challenge lililochezwa jana uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Timu hizo zilitoka sare ya 0 - 0.
Matokeo ya Mechi Zanzibar Heroes na Burundi Amavubi

Benchi la Timu ya Zanzibar likiangalia mchezo unaoendelea kati ya Timu ya Zanzibar na Burundi ambapo timu hizo zilishindwa kufungana
Kocha Msaidizi Abdilatif Abass (kulia) akipeana ushauri na Kocha Mkuu Hemed Suleima (Morocco)O)
Mwamuzi kutoka Rwanda Hudu Munyemana akimtaka Nahodha wa Burundi Ndikumana Yamini kuchagua upande wa shilingi huku Nahodha wa Zanzibar Nadir Haroub ( Cannavaro) akishuhudia.

Picha zote na Haroub Hussein

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.