Doris Maliyaga
KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya Visiwani (Zanzibar Heroes), Stewart Hall ameitwa kuendelea na kazi ya kukinoa kikosini hicho kinachoshiriki michuano ya Kombe la Chalenji inayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Stwart ambaye pia ni kocha wa klabu ya Azam FC, alisimamishwa na uongozi baada ya kushindwa kujiunga na timu ilipokuwa ikifanya maandalizi ya kushiriki michuano hiyo nchini Misri.
Hatua ya kumsimamishwa kwake ilikwenda sambamba na kumteua wa timu ya taifa ya vijana, Karume Boys Abdul Abbas.
Ofisa habari wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Muniri Zakaria amesema jana kuwa, kocha huyo alijiunga na timu mwanzoni mwa wiki iliyopita.
"Stewart amerudi rasmi kuifundisha Zanzibar Heroes na tayari ameshaanza kazi yake tangu juzi (mwanzoni mwa wiki)," alisemaalieleza Muniri.
Kurejea kwa Hall kumepelekea kocha Abbas kurudishwa Zanzibar kuendelea na majukumu mengine.
Zanzibar ilianza michuano hiyo kwa kichapo cha mabao 2-1 toka Uganda, na kisha kwenda sare ya bila kufungana na Burundi.
No comments:
Post a Comment