Na Marzuk Khamis Maelezo Pemba
Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Tawi la Pemba limetakiwa kuziangalia kwa kina Fedha zao wanazowapa Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC) kutokana na fedha hizo kuwa ni chakavu na hazifai kuwapa Wakulima wanaouza Karafuu zao katika vituo mbali mbali vya ununuzi wa Karafuu kisiwani Pemba.
Wakitembelea vituo vya ununuzi wa Karafuu leo Wajumbe wa kamati ya kitaifa ya zao hilo ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja Mustafa Mohamed Ibrahim wameelezwa hayo wakati walipokuwa wakivitembelea vituo mbali mbali vya ununuzi wa Karafuu viliopo katika Mkoa wa Kaskazini na Kusini Pemba kwa kutaka kujua hali ya ununzi wa karafuu na changamoto waliokuwa nazo.
Wakuu wa vituo mbali mbali vya ununuzi wa Karafuu wamesema kuwa baadhi ya Fedha wanazopewa kutoka Benki ya Watu wa Zanzibar kwaajili ya malipo ya Wakulima mara baada ya kuuza Karafuu zao huwa zimechakaa kwa hivyo wanashindwa kuwalipa wakulima .
Katika kituo cha Finya jumla ya shillingi millioni mbili ziligundulika zimechakaa na kushindwa kuwalipa wateja wa zao la Karafuu wanaokwenda kwa ajili ya kuuza Karafuu zao na kusababisha usumbufu kwa wateja hao japo kuwa Fedha hizo zinaporudishwa katika Benki hiyo hukupokelewa na kupewa Fedha nyengine.
Hata hivyo Wakuu hao wa Vituo wamewaomba viongozi wa Benki hiyo ya watu wa Zanzibar Tawi la Pemba kulifanyia kazi tatizo hilo licha ya juhudi zao na jitihada kubwa wanazozichukuwa katika utekelezeji mzuri wa Kutoa Feha hizo..
Wakizungumzia suala la Mvua kubwa inayoendelea kunyesha hivi sasa Kisiwani Pemba wamewaomba Wazazi kuacha tabia ya kuwatuma watoto wao kuuza Karafuu kwani hupelekea kuleta migongano hasa ya vipimo wakati Karafuu hizo zinapopimwa huonekana kiwango chake kimetafautiana kati yao na Mkulima anayeuza Karafuu.
Wakuu wa vituo hao wa ZSTC wamesema kuwa hivi sasa ni msimu wa Mvua za Vuli na kutokana na Mvua hizo kuendelea kunyesha ,Karafuu hushindwa kuikauka mara moja hivyo zinapunguwa uzito wake kutokuwa na ukosefu wa jua. Wajumbe wa Kamati hiyo ya Taifa ya Kusimamia zao la Karafuu Zanzibar walitembelea vituo vya Kengeja,Mtambile,Chumbageni Wambaa na kituo cha Madungu viliopo katika Mkoa wa Kusini Pemba ambapo hapo jana kamati hiyo ilitembelea vituo kama hivyo katika Mkoa wa Kaskazini Pemba.
No comments:
Post a Comment