Na Haroub Hussein
CHAMA cha Soka Zanzibar (ZFA), kimesema kuzuiwa kwa paspoti za wachezaji wa Zanzibar Heroes walioko katika timu ya Taifa Stars, kulilenga kuepusha usumbufu wakati wa mechi ya kufuzu fainali za Kombe
la Dunia dhidi ya Chad.
Tahir alikuwa akijibu masuala ya waandishi wa habari katika mkutano wa jana uliofanyika kwenye ofisi za chama hicho hoteli ya Bwawani.
Alifahamisha kuwa, katika mashindano ya kimataifa, paspoti za wachezaji ndizo zinazotambuliwa kuwa leseni, na hivyo ni lazima ziwasilishwe wakati wa mechi maalumu kama za Kombe la Dunia.
Awali, mmoja wa viongozi wa ZFA aliyeambatana na timu ya taifa ya Zanzibar ‘The Zanzibar Heroes’ nchini Misri, alikaririwa akiilaumu TFF kwa kitendo cha kuzizuia paspoti hizo, huku visa za safari zikiwa
hazijapatikana.
Akitoa ufafanuzi, Tahir alisema, kwa kutambua umuhimu wa timu ya Taifa ya Tanzania, ZFA haikuona sababu ya kuwang’ang’ania wanandinga wake wa Zanzibar kwenda Misri mapema pamoja na waliotangulia, na kwamba sasa wanajiandaa kuondoka kesho baada ya mchezo wa marudiano kati ya Taifa Stars na Chad unaotarajiwa kuchezwa leo kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Alisema ZFA imetuma vivuli vya paspoti hizo kwa TFF ambayo iliahidi kuzigongesha visa, na kwamba zinashughulikiwa na ofisa wake mmoja aliyepelekwa huko makusudi kuhakikisha hilo linafanyika.
Kuhusu kocha mkuu Stewart John Hall, ambaye alikwama kusafiri Novemba 10, baada ya paspoti yake kubainika imejaa na kukosa sehemu ya kugonga visa, alisema ni matarajio ya chama chake kuwa mwalimu huyo naye ataondoka pamoja na wachezaji hao baada ya mchezo wa leo kwa kutumia paspoti ya muda aliyoahidiwa kupewa na ubalozi wa Uingereza uliopo Dar es Salaam.
Wachezaji hao wanaotarajiwa kuungana na wenzao jijini Cairo kabla mashindano ya Chalenji yaliyopangwa kuanza Novemba 25, jijini Dar es Salaam, ni nahodha Abdi Kassim ‘Babi’, msaidizi wake Nadir Haroub
‘Cannavaro’, Nassor Masoud ‘Cholo’ pamoja na mlinda mlango Mwadini
No comments:
Post a Comment