Mchezaji wa timu ya Ngome Hadidi Shaame (kulia) na mchezaji wa timu ya Sharp Boys Hija Haji, wakiwania mpira ukiwa katika moja ya dimbwi la maji lililokuweka katika uwanja huo, katika mchezo wa ligi daraja la kwanza Zanzibar mchezo uliofanyika uwanja wa Mao, timu ya Ngome imeshinda.2-0.
Uwanja ukiwa umetawaliwa na maji sehemu kubwa ya uwanja huo na kuwafanya wachezaji kuwa na kazi ya ziada, mpira unapotuwama katika maji.
Mshambuliaji wa timu ya Sharp Boys ya Nungwi,Hija Haji akimpita beki wa timu ya Ngome Salum Omar, katika mchezo wa ligi daraja la kwanza Zanzibar uliofanyika uwanja wa Mao, ukiwa na maji yanayotokana na mvua zinazoendelea kunyasha.
Kizaza katika goli la timu ya Ngome, katika mchezo wa Ligi Kuu Daraja la Kwanza Zanzibar, uliofanyika uwanja wa Ma, timu ya Ngome ya Fuoni imeshinda 2-0.
AIBU GANI HII??!
ReplyDeleteYAANI HUO NDO UWANJA UNAOCHEZEWA 'LIGI KUU'?!
SIJAPATA KUONA DUNIA NZIMA.
KWA MSINGI HUU,NCHI IUZWE NA KILA MMOJA AGAIWE CHAKE!
Huu mpira au vanga?kama vipi si muisimishe tu iyo ligi mpaka mvua zipite. kweli tunatarajia kutoa viwango apo?nahisi kama tutaendelea vile vile tu kusema kama si kipa ingekua goli.
ReplyDeleteMatatizo ya muungano hayo..yakhe!
ReplyDelete