Na Hadia Khamis
MAMLAKA ya mapato Tanzania (TRA) kanda ya Zanzibar imefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 33.5 tokea juni hadi Novemba, 2011
Mapato hayo ni ni ongezeko kubwa kutoka mapato ya kipindi kma hicho mwaka jana, ambapo Mamlaka hiyo ilikusanya shilingi bilioni 28.
Akitoa taarifa hiyo, Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Kanda ya Zanzibar, Mcha Hassan, alisema mamlaka hiyo ilitakiwa ikusanye zaidi ya shilingi bilioni 100.58 ktika kipindi cha mwaka wa fedha uliomalizikia Novemba, 2011.
Alimueleza mwandishi wa habari hizi alipomtembele ofisini kwake Msikiti Mabuluu kwamba kiwango cha shilingi bilioni 33.5 kilichokusanywa na Mamlaka yake ni kikubwa kulinganishwa na mwaka uliopita.
Alisema zipo sababu mbili kubwa zilizochangia kupungua kwa mapato kati ya mwaka huu na mwaka jana, alisema ilitokana na baadhi ya taasisi za serikali ya Muungano ziliopo Zanzibar kushindwa kujlipa kodi ya shilingi bilioni 1.5.
Hata hivyo, aliwataka walipa kodi wote wanaopitia Mamlaka hiyo kuacha tabia ya kuchelewesha kufanya malipo hatua ilioyoelezwa inachelewesha utaratibu.
No comments:
Post a Comment