Habari za Punde

WFP YAKABIDHI VIFAA VYENYE THAMANI YA MILIONI 51 KWA WIZARA YA KILIMO NA MALIASILI


Na Hamad Hija Melezo Zanzibar

Shirika la Chakula Duniani (WFP) limekabidhi msaada wa vifaa mbali mbali vyenye thamani ya Shl.Million 51 kwa Wizara ya Kilimo na Maliasili Zanzibar ili viweze kusaidi Wizara hiyo katika kufanya vyema majukumu yake ya kila siku.

Msaada huo umekabidhiwa na Mwakilishi wa Shirika hilo Richard Ragan kwa Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum Machano Othman Said kwa niaba ya Waziri wa Kilimo na Maliasili Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo hii Maruhubi mjini Zanzibar.



Vifaa ambavyo vimekabidhiwa ni pamoja na Kompyuta ambavyo vitasaidia katika kufanya tafiti mbali mbali zitakazo saidia kuendeleza kilimo na maendeleo kwa ujumla.

Aidha vifaa hivyo pia vitasaidia kufahamisha mwenendo mzima wa masoko duniani, kuchambua bei mbali mbali za bidhaa katika masoko ya ndani na nje ya Zanzibar

Kwa upande wake Katibu wa Wizara ya kilimo na Mali Asili Zanzibar Affan Masoud amelihakikishia Shirika la Chakula Duniani WFP kuwa vifaa hivyo vitatumika vyema kama vilivyo kusudiwa.

Aidha Katibu huyo wa Wizara ya Kilimo na Mali asili amelishukuru Shirika hilo kwa kuona umuhimu wa kuisadia Zanzibar katika maswala ya kilimo ambacho ndicho Uti wa Mgongo wa Taifa hili.

Affan amelitaka shirika hilo la chakula duniani WFP kuendelea kuisaidia Zanzibar katika masuala mbali mbali yahusuyo kilimo na masuala mengine ambayo yatachangia maendeleo katika taifa

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya shughuli hiyo ya makabidhiano Katibu huyo wa kilimo aliwaambia waandishi wahabari kuwa wizara ipo tayari kutowa taarifa juu ya masuala ya kilimo na waaandishi wawe tayari kuandika taarifa hasa zinazohusu masuala ya kilimo huko vijini

Akizungumzia juu ya kuboresha kilimo amesema kuwa hivi karibuni wameajiri mabwana shamba 110 katika shughuli zao za kuboresha kilimo hata hivyo amesema kuwa mabwana shamba hao hawatoshi kwa mahitaji ya sasa.

2 comments:

  1. Jamani tuache 'ukasuku' (kuiga iga kila kitu) Tunaposema kilimo ni uti wa mgongo wa TZA tuna kusudia Bara sio ZNZ! Mm na 'challenge' ni zao gani la chakula linalozalishwa hapa na ambalo, kama tukiacha kuangiza chakula kwa muda wa mwezi mmoja tuu linaweza kutusaidia? Hao 'WFP' hivyo vifaa nawatoe tuu kwa vile ni wajibu wao kama shirika la umoja wa mataifa lkn. si dhani kama itasaidia lolote! Kama hao mabwana shamba 110 watashughulikia kilimo cha aina gani?..tuambiwe! Ukienda kwerekwe asub. utakuta, tungule vitenga 4, vitenga viwili vitatu vya machungwa, vibilingani, mikungu miwili ya ndizi, madalali wanagombania,..iliza bei hapo, anaekula ndizi ZNZ, tajiri! Bora wizara yetu ingeshughulikia kilimo cha mboga mboga tu, tukajua moja na wengine wakapelekwa kule kizimbani, wakasaidia kuboresha lile shamba la viungo tukaonyesha wazungu!

    ReplyDelete
  2. anonymous wa kwanza , inaonesha we hata bustani ya maua huna na pili fani yako hasa ni kuzungusha wazungu kama ulivyo sema mwenyewe , kama kilimo hakuna basi huo msaada utakuwa chachu ya kukianzisha na kukipamashiko miongoni mwa jamii ya wazanzibari ; wote hatuwezi kuwa watembeza wazungu ; japo inaonekana umeacha siku hizi

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.