Habari za Punde

Balozi Seif Azindua Kituo cha Zantel Cha Huduma kwa Wateja - Zanzibar Call Center.

 Jengo la Ofisi za Zanzibar Call Center loikisubiri kuzinduliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Amaani.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel Ali Hamad Bin Jarsh.alipowasili viwanja vya Kampuni hiyo Amani.   
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akisalimiana na Viongozi mbalimbali.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akitoa hutuba katika sherehe za Uzinduzi wa Kituo cha Huduma kwa Wateja, katika Viwanja wa Kampuni hiyo Amaani.  
 Waheshimiwa wakimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akitowa nasaha zake kwa Wafanyakazi wa Zantel.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel Zanzibar Ali Hamad Bin Jarsh, akitowa hutuba ya kampuni yake katika uzinduzi wa Kituo cha Huduma kwa Wateja .katika Majengo ya Kampuni hiyo Amani Maeneo Huru ya Uchumi Zanzibar.
Baadhi ya Wananchi waalikwa wakimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akitowa hutuba yake ya Uzinduzi wa Kituo hicho.    

Afisa wa Zantel akitowa maelezo ya ujenzi wa Kituo hicho na huduma zinazotelewa kwa wateja wea Kampuni ya Simu za Mikononi ya Zantel katika sherehe za Uzinduzi wake.
Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Zanzibar Hamad Masoud,akitowa nasaha zake kwa Wafanyakazi wa Zantel katika sherehe za Uzinduzi wa Kituo cha Huduma kwa Wateja.  

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akizinduwa Jengo la Kituo cha Huduma kwa Wateja -Zanzibar Call Center,  
Ofisa wa Kituo cha Huduma kwa Wateja Omar akitowa maelezo jinsi ya huduma zinazotolewa na kituo hicho kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, baada ya kukizinduwa.  




Wananchi waliofika kushuhudiwa Uzinduzi wa Kituo cha Huduma kwa Wateja wakimsikiliza Ofisa wa Kituo hicho akitowa maelezo ya huduma zinazofanywa katika chumba hicho. 
Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa kampuni ya zantel,baadhi ya Mawaziri na watendaji wa serikali.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizindua kituo cha huduma kwa wateja cha kampuni ya simu za mkononi ya Zantel hapo eneo huru Amani.


Asilimia 42.5% ya pato la Zanzibar kwa mwaka 2010 limetokana na Sekta ya Huduma ambayo ndio inayoongoza katika kulipatia pato kubwa Taifa hili.

Akikifungua Kituo cha huduma kwa wateja cha Kampuni ya Simu za mikononi cha Zantel hapo Maeneo huru Amani Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema uchumi wa Zanzibar kwa asilimia kubwa un aendelea kutegemea utoaji wa huduma.

Balozi Seif alisema yapo mapungufu mengi katika Sekta hii ambayo ni vyema yakafanyiwa kazi kwa maslahi ya Taifa.


Akatolea mfano wa tabia ya kuwavunjia wateja shughuli zao za kimaisha kwa sababu za kuongojea huduma linafaa kuachwa mara moja.

“ Wateja wengi nikiwemo mimi sipendi kusikia neno “subiri” ambalo kwa sana linaonekana kama neno la kawaida kwa watoa huduma kumbe ni adui mkubwa kwa watoaji huduma hiho”.Alitahadharisha Balozi Seif.
Aliushauri Uongozi wa Kampuni hiyo kusikiliza malalamiko ya wateja kwa lengo la kuepuka mivutano isiyo ya lazma baina ya Kampuni ya Wateja wao.

Balozi Seif pia aliiomba Kampuni hiyo kuendelea kuwajali wateja wao wa Zanzibar ambao ndio waliifundisha tata Zantel na sasa Kampuni hiyo inakimbia kwa haraka.

Katika Salamu za Uongozi wa Kampuni ya Zantel zilizosomwa na Bibi Shinuna Kassim kwa Niaba ya CEO wa Zantel Bwana Ali Hamad Bin Jarsh wamesema uzinduzi huo unakirudisha kituo cha Zantel huduma kwa Wateja nyumbani kwao.

“ Waswahili wanasema Mtu kwao na hii ingekuwa sababu tosha ya kukirudisha kituo hichi nyumbani ”. Alifafanuwa Bibi Shinuna Kassim.

Alisema kamba lengo kuu la kukirudisha kituo hicho Zanzibar ni kuongeza ajira kwa Vijana, Kukuza Kiwahili sanifu kwa wateja wanaotumia Zantel pamoja na kupunguza gharama na kubadilishana faida baina ya mashirika na Makampuni ya Serikali .

Mapema akimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Waziri wa Mawasiliano na Miundo Mbinu Mh. Hamad Masoud ameihakikishia Kampuni ya Zantel kwamba Serikali itakuwa pamoja nao katika kuhakikisha huduma bora za Mawasiliano zinawafikia Wananchi.

Mh. Hamad aliishauri Kampuni hiyo ya Zantel kuheshimu Mikataba ya Kazi kwa Wafanyakazi wao ili kuondosha malalamiko yanayojitokeza kwa baadhi ya Wafanyakazi hao.


Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
25/1/2012.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.