Habari za Punde

MAPINDUZI CUP YAZIDI KUPAMBA MOTO UWANJA WA AMANI KATI YA SIMBA NA MIEMBENI UNITED.

 Waziri wa Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo Abdillah Jihad na Makamu Mwenyekiti wa Mapinduzi CUP, Shery Khamis, wakipigwa na butwaa matokeo ya mchezo kati ya Simba na Miembeni United.  
Mfadhili wa timu ya Miembeni United Amani Makungu, akifuatilia mchezo huo unavyoendelea kwa upinzani wa hali ya juu na kuonesha kiwango timu yake.  
Mchezaji wa timu ya Miembeni United Ibrahim Khamis,akimiliki mpira huku mabeki wa timu ya Simba wakijaribu kumnyanganya, katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi uliofanyika uwanja wa Amani timu ya Simbqa imeshinda 4-3  
Kipa wa timu ya Simba Ali Mustafa, akiokowa moja ya mashambulizi golini kwake.    
Wapenzi wa mchezo wa soka wakifuatilia mchezo wa Simba na Miembeni United uliofanyika jana usiku, ulikuwa na upinzani wa hali ya juu  hati kwa timu hizo mbili. 
Mshambuliaji wa timu ya Simba Felix Sunzu(kushoto) na beki wa timu ya Miembeni United Azizi Shaweji, wakiwania mpira katika mchezo wa Mapinduzi Cup.timu ya Simba imeshinda 4-3 
Mshambuliaji wa timu ya Simba Felix Sunzu, akimpita beki wa timu Miembeni United Soud Abdi.
Mshambuliaji wa timu ya Simba Haruna Moshi, akimpiga chenga beki wa timu ya Miembeni United Emmanuel Albert.(kulia)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.