Habari za Punde

Mdau Anaulizia Website ya TVZ Kulikoni?

Assallam Alaykum kaka

 Naomba utupashie habari hapo nyumbani kwa viongozi yoyote anaehusika au hata wewe mwenyewe ukiwa unamjua muhusika mkuu. Kwa kweli sisi tuliokuwa mbali na nyumbani hupenda sana kupata habari za kwetu sasa inakuwa maajabu unaangalia website ya Television Zanzibar last update yake tangu Mh.Shein anachukua fomu mpaka leo hii wameshindwa kuweka update zozote.

Kama wanaweza watupe kazi sisi tutawafanyia bila ya hata malipo tupo vijana tunataka kujitolea
ahsante

Mungu Ibariki Zanzibar

2 comments:

  1. Ningependa kuongezea khs hili jambo si TVZ tu ila niliangalia kuna siku,hata ukisearch mfano serikali ya mapinduzi ya zanzibar official website hakuna kitu,aibu gani serikali nzima haina hata website, niliwahi hata kumuandikia muwakilishi mmoja kumwambia hebu angalau zungumzia kuhusu hili jambo kuwa serikali,iwe na website ambayo inafanya kazi ila hamna kitu naona kimya. ila wacha turudi kwenye TVZ hawa jamaa wameozaa hawafai pesa mbili ila pia tuseme ukweli kitu kimoja kinachangia kuwekana tu kwa watu wasiokuwa na elimu na kupachikizana wenyewe kwa wenyewe ndio maendeleo yakawa duni.

    ReplyDelete
  2. Nawashkuru sana: muuliza swali na mtoa maoni wa kwanza kwa namna mnavyoonyesha uchungu juu ya maendeleo ya visiwa vyetu. Kama ninavyosema kila siku, lau kama watu wangekua wanatembelea mtandao huu kikamilifu(pamoja na viongozi) kwa kweli tungekua mbali.

    Mimi, wakati mwengine hufikiria na kujiuliza maswali kuhusu mambo yanavyokwenda visiwani mwetu mpaka ikafikia mahala nikajishuku nikasema'isije ikawa nazungumzia mambo nisiyoyajua'..maana wasomi na viongozi wetu..kimyaa!!

    Wakati mwingine, hukaribia kuunga mkono yale maneno ya wenzetu kutoka upande wa pili wa jamuhuri wanapodai 'waz'bari hatukusoma' kwasababu kusoma sio kuwa na vyetu tu, bali kua 'active, challenging and visionary' ili kuleta maendeleo.. lakini wapi?

    visiwa ambavyo vimenufaika na elimu bila malipo kwa takriban miaka 38 ya uhuru wetu, leo hii tulitarajia tuwe na wataalamu wengi wa kizanzibari ktk sehemu mbali mbali za jamhuri yetu, afrika mashariki na dunuani..lakini wapi..?na ukiuliza hapo..utaskia..'muungano wanatubane'

    Tukija kwenye TV, tulitarajia Wazenj wengi leo hii wangekua ni wataalamu na watangaazaji kwenye vituo mbali mbali vya televisheni nchini kwa vile sisi tulikua wa mwanzo kumiliki mtambo huo.. lakn. wapi?..tunaringia MARIN HASSAN tu.
    Hata tasnia ya filamu tulitarajia tuwe tunaongoza na sio kina KANUMBA kwa vile kituo cha TV na mambo ya maigizo ya filamu huenda sambamba..lakini wapi?

    Siku moja nilikua naangalia mdahalo chuo kikuu cha SUZA, mw'funzi mmoja alisimama kutoa maoni, kwa kweli.. nilisikitika,..nikasema kama wasomi wenyewe ndio hawa wanaokuja kuongoza taasisi zetu mbali mbali basi bora DIV.4 yangu ya FORM6!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.