Habari za Punde

Taarab Rasmi Kusherehekea Miaka 48 ya Mapinduzi

Mwimbaji Fatma Issa wa Kikundi cha Culture Muzical Club akiwaburudisha mashabiki katika ukumbi wa Slama Bwawani kwa nyimbo ya "Umewashika" katika sherehe za Kutimiza miaka 48 ya Mapinduzi ya
Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akiangalia taarab Rasmi iliyocharazwa na Kikundi cha Culture Muzical Club katika Ukumbi wa Salama Bwawani katika
kusheherekea Miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar,(wa kwanza kulia) Mama Balozi Seif Ali Iddi,Mkuu wa Mkoa wa Mjini Mahgaribi Abdalla Mwinyi Khamis na (kushoto) Waziri wa habari Utamaduni na Michezo Abdilah Jihadi Hassan.
Wasanii wa kikundi cha muziki cha Culture Musical Clib wakicharaza ala katika hafla maalum ya kusheherekea miaka 48 ya Mapinduzi Zanzibar katika ukumbi wa Salama Bwawani 

Picha na Ramadhan Othman, Ikulu

1 comment:

  1. Mar..habaa!! Ama kweli siasa ndio kila kitu, yaani mara tu baada ya mabadiliko ya kisiasa Z'bar sasa kila kitu kina rudi upya?

    Mimi nakumbuka mambo ya taarab rasmi hatukuyaona visiwani kwa takriban awamu mbili zilizo pita.
    Sasa naamini hata 'nadi ikwan swafaa(malindi) itarudi kwenye chati.

    Utamaduni ni moja ya kivutio cha utalii, na taarab imesaidia sana kuitangaza Z'bar kiutalii.
    Kuna watalii wengi wanapokuja Z'bar huulizia kama wanaweza kuhudhuria angalia tamasha moja la taarab lakini huishia kupigwa bla..bla.

    Nakumbuka niliwahi kukutana na mama mmoja wa kimarekani takriban miaka 2 iliyopita, akaniambia yupo kwenye utafiti kuhusu muziki wa taarab asilia ambapo ameambiwa kwa sasa unapatikana tu; Misri na Z'bar na hivyo nikamsaidia kukutana na bwana mmoja anaitwa CHIMBENI KHERI sijui tena walifikia wapi lakini kwa kweli tukiwa srious bado 'oportinities' zipo.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.