Na Khamisuu Abdallah
IDARA ya Uhamiaji Zanzibar mwaka jana, iliwatia nguvuni watu 39 waliokuwa wakiishi Zanzibar kinyume cha sheria.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake Miembeni mjini hapa, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Neema Mashaka Shaji alisema wahamiaji hao wamechukuliwa hatua mbali mbali.
Miongoni mwa hatua zilizochukuliwa dhidi ya wahamiaji hao haramu ni pamoja na kupandishwa kizimbani kujibu mashitaka ya kuvunja sheria za uhamiaji.
Naibu huyo alibainisha kuwa hatua nyengine zilizochukuliwa na Idara yake ni kuwarejesha nyumbani baadhi ya wahamiaji hao.
Alisema hivi sasa uhamiaji haramu kwa kiasi umepungua hapa Zanzibar, hali iliyosababishwa na wananchi kuwa na elimu na ufahamu wa kuwatambua wahamiaji haramu.
Alifahamisha kuwa wahamiaji wengi waliokamatwa katika kipindi hicho ni wale waliopewa vibali vya ukaazi wa muda, ambapo baada ya kumalizika muda wake huendelea kuishi nchini jambo ambalo ni kinyume na sheria.
“Wageni wengi tunaowakamata wakivunja sheria za uhamiaji ni wale wanaoendelea kuishi nchini huku vibali vyao vya kuishi vikiwa vimeshamaliza muda, ambapo hatua tunayoichukua dhidi yao ni kuwarejesha kwao”,alisema Naibu huyo.
Naibu huyo alisema Idara yake hivi sasa inakabiliwa na changamoto mbali mbali katika kufanikisha majukumu yao ikiwemo gari, vipando vidogo vidogo kama honda, vespa na boti kwa ajili ya ulinzi baharini.
Naibu huyo aliwaomba wananchi kuwa makini kuwabaini wahamiaji haramu na kutoa taarifa kwa Idara yake na mamlaka nyengine ili hatua za kisheria dhidi yao zichukuliwe.
Aidha alivitaka vikosi vya ulinzi kuzidisha mashirikiano baina yao ili kukomesha suali la uhamiaji haramu.
PASSPORT IKO WAPI ZANZIBAR AMKA RUDIUSHA PASS VUNJA MUNGANO TUSHASHOKA NA WALE WANZANZIB AR WALIOKO BARA WARUDI MAKWAO UCHUNGU MNATAKA KANDA YA BAHARI MTARISTIMA MAJINI MUWEHUKE NYINYI NA VIONGOZI WENU WA NZANZIBAR SI MUNAWATUMILIA HAWA KINA SHAMUHUNA MWENYEWE KESHAWEHUKA ANNA TIBAIJOKA HILI LAANATUL IKUSHUKIE
ReplyDelete