Habari za Punde

Mafunzo Yaondoka Kwenda Kuivaa Timu ya Msumbiji - Yaahidi Ushindi

KIKOSI cha watu 25 wakiwemo wachezaji 18 na viongozi saba wa mabingwa wa soka Zanzibar timu ya mafunzo, kinaondoka nchini leo kuelekea Msumbilji, tayari kwa mchezo wa marudiano wa ligi ya Mabingwa barani Africa dhidi mabingwa wa soka ya Msumbiji Muslimana De Maputo utakaopigwa Machi 10 huko nchini Msumbiji.

Katika msafara wa timu hiyo ambayo inaondoka kwa boti asubuhi hii kwenda Dar es Salam na kupanda ndege ya shirika la Air Msumbiji saa 11 jioni na kuwasili Msumbiji saa 2:45 za usiku, ambapo timu hiyo ili iweze kusonga mbele inatakiwa ishinde zaidi ya magoli 3 -0.


Hafla ya kuwaanga wachezaji hao na kukabidhiwa bendara ya Zanzibar ilifanyika katika ukumbi wa bwalo la vyuo vya Mafunzo Kilimani, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Ali Mwinyikai, pamoja na viongozi wengine wa baraza la michezo Zanzibar, ZFA na viongozi wa jeshi la Mafunzo.

Akitoa nasaha zake kabla wa kukabidhi bendera ya kwa nahaodha wa timu hiyo Katibu huyo aliiwataka wawakilishi hao kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha wanafanya vyema, kwa lengo la kuiletea sifa Zanzibar kwani huko wanakwenda kupeperusha bendera ya Zanzibar.

‘’Huko mnakwenda kushindana la msingi ni kuelekeza nguvu zenu katika mchezo huo ili muweze kufanya vyema, kwani ushindi wenu utaileta sifa Zanzibar, na katika kufanikiwa hilo lazima kwanza mujiamini’’alisema.

Alisema kuwa hivi sasa serikali kupitia Wizara ya Michezo iko katika mikakati ya kuifanya Zanzibar timu zake zote zinafanya vyema, hivyo ni vyema kwa timu ya Mafunzo ikawa ni ya mwanzo kutekeleza hilo.

Kwa upande wake Kamishna wa vyuo vya mafunzo Zanzibar Khalifa Chuom ameishukuru kamati ya kuendeleza michezo Zanzibar KUMIZA, kwa jitihada zake ilizozichukuwa kwa kufanikisha safari hiyo, na kuwataka wachezaji hao kucheza kwa kujiamini ili kuweza kushinda mchezo huo.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake nahodha wa mabingwa hao Haji Mwambe Ramadhani,alisema licha ya kupoteza mchezo wao wa mwanzo watajitahidi kucheza kwa jihadi ili waweze kushinda mchezo huo.

Hivyo amewataka Wazanzibar kuwapa ushirikiano kwani uwezo wa kwenda kushinda ugegeni upo, licha ya baadhi ya watu kuanza kupoteza matumaini na timu yao, lakini wakumbuke mpira wa miguu hawezi kutabirika.

Msafara wa timu ya Mafunzo viongozi ni Hassan Haji Haji ambaye ni kiongozi wa msafara, Katibu Makame Faki ( katibu) Hemed Moroko (meneja) Mohammed Kachumbari ( kocha Mkuu), Mussa Soraga ( mjumbe ZFA) na Kibata Haji Daktari wa timu.

Kwa upande wachezaji watakaopanda pipa ni Salum Mohammed, Suleiman Janabi, Haji Abdi, Mbarouk Zahran,Said Mussa, Yussuf Makame, Haji Ramadhani, Wahid Ibrahim, Maulid Mussa na Kheir Salum.Wengine ni Mohammed Mbambi, Ali Juma, Sadik Habib, Jaku Joma, Bakari Ayoub, Zahoro Salmin, Fikirini Rajab na Saleh Ali

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.