Habari za Punde

Mkutano wa Saba wa Baraza la Wawakilishi Kuanza kesho.

 Mkutano wa saba wa Baraza la Wawakilishi unatarjiwa kuanza Jumatano  ambapo pamoja na mambo mengine utajadili Miswada saba ya sherina na hoja binafsi moja pi aitawasilishwa.

Kaimu Katibu wa Baraza la Wawakilishi Bw Mdungi Makame Mdungi akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ameitaja Miswada itakayojadiliwa ni pamoja na Mswada wa sheria ya Kufuta Sheria ya tume ya Mipango No 5 ya mwaka 1989 kwa ajili ya uendeshaji tume hiyo


Mengine ni Mswada wa Maslahi ya Viongozi wa Kisiasa wa mwaka 2012, Mwada wa Sheria ya kuanzisha Taasisi ya utafiti wa Kilimo, Mswasa wa kuanzisha Taasisi ya utafiti wa Kilimo, Mswada wa Sheria ya kuanzisha mfuko wa maendeleo YA Jimbo na mswada wa marekebisho ya Sheria ya Utalii No6 mwaka 2009.

Bw Mdungi amefahamisha kuwa hoja binafsi ni kuhusu kuundwa kwa kamati teule ya kuchunguza matatizo mbalimbali ya Shirika la Umeme ( Zeco) itakayowasilishwa na mwakilishi wa Jimbo la Kiwani Mhe Hija Hassan Hija.

 Katika kikao hicho jumla ya masuali na majibu 153 yataulizwa na kupatiwa majibu

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.