Habari za Punde

Umoja wa Wananchi wa Tanga Zanzibar wapata Uongozi Mpya

Umoja wa  Watu wa Tanga wanaoishi Zanzibar umefanya Uchaguzi wa Mwaka kuwachagua Viongozi mbalimbali watakao uongoza umoja huo katika kipndi hichi.


Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi wa umoja huo Bw Titus Shemauwa amesema nafasi nane zimegombewa katika uchaguzi huo Bw Hersow Nyenga Shekibarazi amechaguliwa kuwa Mwenyekiti kwa kupata kura 148 na kumshinda mpinzani wake Bw Adam Hassan Kinyanga aliyepata kura 100.

Amesema Bw Shaaban Mang’enya amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu Bw Zamir Shekhe Mtumwa, Msaidizi Katibu Bw Amir Yussuf Kingazi, Mhasibu Mkuu Bw Juma Hussein, Msaidizi Mhasibu Zaniar na Wajumbe wawili ni Bi Amina Salum Sleiman na Mwanamvua.

Nae Mwenyekiti  amewataka Wanachama wa Umoja huo kuridhia yale yote yaliyopitishwa kwa mujibu wa Katiba ili kuimarisha umoja huo.

Amesema Kiongozi mzuri ni yule anaekubali kukosolewa na kuthamini mawazo ya wengine hivyo yuko tayari kufanya hivyo ili kuundeleza umoja huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.