Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dk Omar Dadi Shajak amesema ipo haja ya kuwepo kwa mageuzi katika vyombo vya habari kutoka Analogi kwenda Digital ili kufanikisha mabadiliko makubwa katika Teknolojia ya Mawasiliano Zanzibar..
Amesema kuwa Zanzibar likiwa ni Taifa linawajibu wa kutekeleza kikamilifu na mabadiliko ya Teknolojia yanayotokea Duniani ambapo kutochukuliwa hatua hiyo kutaweza kuwaacha nyuma wananchi wa Zanzibar katika sekta ya habari.
Akifungua Mafunzo ya siku tano juu ya mageuzi ya Teknologia kwa Mameneja wa Vituo vya Utangazaji katika Ukumbi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar amesema mafunzo hayo yatawapatia taaluma ya kutosha katika kukabiliana na changamoto kadhaa.
Amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuzingatia kikamilifu kwa kujielimisha ili kwenda na wakati kwa kubadilisha utendaji katika vituo vyao.
Nao washiriki wa mafunzo hayo wamesema yatawasaidia kwa kuendesha vipindi vizuri vinavyoweza kuhimili ushindani katika Radio na Televisheni pamoja na kuleta mabadiliko katika jamii.
No comments:
Post a Comment