Habari za Punde

Ziara ya Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein Mkoa wa Mjini Magharibi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein, akikabidhiwa CD za nyimbo mbali za Qusida zilizotengenezwa na Vijana Wajasiriamali wa Kwahani, wakati wa kusomewa risala ya Utekelezaji ya Mkoa wa Mjini Magharibi katika ukumbi wa Ofisi yac Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi.
 Viongozi mbalimbali wa Serekali wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi akiwasilisha  risala ya utekelezaji ya Mkoa wake kwa kipindi cha miezi mitatu.na malengo ya mkoa. 
 Wanafunzi wa Skuli ya Kianga Mkoa wa Magharibi wakisoma Kuran wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la Madarasa yao manne  mapya.  
 Mwanafunzi Maryam Ali, akisoma utenzi katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la madarasa yao mnne maya yakiwa katika hatuwa ya mwisho ya ujenzi wake.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein, akiwahutubia Wananchi wa Jimbo la Dole katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la madarasa mapya ya skuli hiyo.
 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi akitowa nasaha zake kwa wazee wa Skuli ya Kianga katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi.
 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Abdalla Ramadhan Shaban, akizungumza na Wazee na Wanafunzi wa Skuli ya Kianga wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la majengo mapya ya skuhiyo yanayojengwa kwa nguvu za Wananchi na Mbunge na Mwakilishi. 
 Mwalim Chum Khamis akisoma risala ya skuli hiyo katika eherehe za uwekaji wa jiwe la msingi na kutowa malalamiko yao ya kuchelewa kuwekea umeme kutoka na transfoma kuwekwa mbali na eneo la skuli hiyo. 

Wanafunzi wa skuli ya Kianga wakiwa katika viwanja vya skuli hiyo wakimsikiliza Rais wa Zanzibar alipofika kuwawekea jiwe la msingi la madarasa mapya ya skuli hiyo.
Wazee wa Kamati ya Skuli ya Kianga wakimsikiliza Rais wa Zanzibar akiwahutubia baada ya kuweka jiwe la msingi.  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein, akiwasili katika viwanja vya Selemu kwa ajili ya Uzinduzi wa Kisima kipya cha maji kwa ajili ya Wananchi wa majimbo matatu ya Dole, Mfeneseni na Bumbwini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein, akizinduwa Kisima kipya cha Maji Safi na Salama, kilichoko katika maeneo ya Selemu. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein, akiwahutubia Wananchi wa Selemu baada ya kuzinduwa Kisima kipya cha Maji kwa ajili ya Wananchi wa majimbo matatu. na kunufaisha shehia 56, kupata huduma hiyo.
Waziri wa Ardhi Maji Makaazi na Nishati Ali Juma Shamuhuna, akitowa nasaha zake kwa Wananchi wa Selemu baada ya kuzinduliwa mradi wao wa msaji sadfi na salamu.ikiwa ni moja ya sherehe za maadhimishioya siku ya maji Duniani.  
Mwakilishi wa Shirika lisilo la Kiserekali la ACRA Andrea Stegagno, akitowa salamu za shirika lake katika sherehe za uzinduzi wa mradi wa kisima kipya cha  maji kilioko katika kijiji cha selemu, ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Maji Duniani.


Mkurugenzi wa Shirika la Maji Zanzibar Mustafa Ali Garu, akitowa maelezo ya Tangi jipya la maji lililopo katika kijiji cha Kama, wakati wa Rais wa Zanzibar alipotembelea na kuzinduwa mradi wa maji safi na salama.     

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.