Habari za Punde

Balozi Seif Ali Iddi Atembelea Ujenzi wa Skuli ya Kinduni.

 Mbunge wa Jimbo la Kitope ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipolikagua Jengo jipya la Skuli ya Msingi ya Kinduni iliyombo ndani ya Jimbo la Kitope. Jengo hilo tayari limeshaezekwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi, akipata maelezo ya maendeleo ya Ujenzi wa madarasa ya Skuli ya Msingi kinduni kutoka kwa Sheha wa Shehia ya Kinduni Ali Ameir Khamis, kuhusu Ujenzi wa Jengo jipya la Skuli ya Msingi Kinduni. linaloendelea na ujezi wake katika shehia hiyo kuondoa upungufu wa madarasa katika jimbo hilo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi Baskeli Tatu Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B. Nd Vuai Ali Vuai kwa ajili ya kuwapatia Walimu watatu wa Skuli ya Msingi ya Kidagoni Jimbo la Nungwi.
Baskeli hizo ni ahadi yake aliyoitoa wakati wa ziara yake ya Mkoa wa Kaskazini Unguja mapema mwezi Machi mwaka huu wa 2012.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, ambae pia ni mbunge wa jimbo la Kitope akimkabidhi zawadi Mwanafunzi  Zubeir Khamis aliyefaulu kuingia Michepuo katika  Skuli ya Mahonda.akitimiza ahadi alizotokwa kwa Wanafunzi watakaofanya vizuri katika mitihani yao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.