Habari za Punde

Dk Shein Ziarani Pemba

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein kesho anatarajiwa kuwasili Kisiwani Pemba kwa Ziara ya siku tano kwa ajili kuangalia utekelezaji wa kazi za Maendeleo Kisiwani humo.

Kwa mujibu wa ratiba iliotolewa na Afisi za mikoa miwili ya Pemba,Mh Rais ataanza ziara yake katika Mkoa wa Kaskazini Pemba kwa kupokea Taarifa ya utekelezaji ya Mkoa huo na baadae ataelekea Mtemani ambapo atazindua Mpango wa Kuanzisha Benki ya Jamii.


Dk Shein atakutana na kuzungumza na Wakuu wa Wilaya, Masheha na Walinzi walioshiriki katika uvunaji wa Karafuu Msimu huu huko katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi uliopo Wete.

Mchana Rais wa Zanzabar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akiwa Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM ataweka Jiwe la Msingi katika Tawi la CCM Bopwe Magharaibi na baadae kuzungumza na wana CCM..

Siku ya Jumaane katika Mkoa huo Mheshimwa Rais atakaguwa Tuta la kuzuiya Maji Chumvi la Bonde la Mkele ambapo atapokea maelezo na kusalimia na Wakulima.

Asubuhi hiyo hiyo Rais ataelekea katika kituo cha Afya Chimba na kuweka Jiwe la Msingi la Kituo hicho na Kupata Maelezo yake.


Aidha mchana Dk Shein atatowa zawadi kwa Wakulima Bora na Kuwahotubia Wananchi huko Katika Viwanja vya ukumbi wa Jamhuri Wete .

Jioni Rais ataweka jiwe la Msingi Tawi la CCM Kinyasini na baadae Tumbe ambapo pia atapata kuwasalimia Wanachama wa CCM.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo Siku ya Jumaatano Mheshimiwa Rais atashirikiana na Wananchi katika upandaji wa Miche ya Mikarafuu katika Shamba la Miikindani Wete ambapo siku hiyo hiyo atafanya majumuisho ya ziara yake katika Mkoa huo.

Kwa upande wa Mkoa Kusini Pemba Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein siku ya Alkhamis ataanza ziara yake kwa kupokea taarifa ya utekelezaji ya Mkoa huo na kufanya ziara katika maeneo mbali mbali yakiwemo Chambani,Ukutini, Michenzani na Makombeni ambapo mote humo atatembelea Miradi ya Wananchi na Kuweka Mawe ya Msingi.

Jioni Dkt Shein ambae pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM atatembelea Tawi la CCM Mwambe na kuzungumza na wana CCM na Wananchi.

Tarehe 20 Mheshimiwa Rais wakati wa Asubuhi atakuwa na Mazungumzo na Kikosi Kazi cha Taifa Kuhusu uvunaji wa zao la Karafuu na baadae kufunga rasmi msimu wa Uvunaji wa zao hilo.

Baadae Rais atakelekea Ziwani kufunguwa Tangi la Maji Ziwani na jioni ataweka Jiwe la Msingi Tawi la CCM Vitongoji la Matungu Changamka na kuzuntgumza na wana CCM pia kutoa kadi kwa wanachama wapya.

Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein anatarajiwa kumaliza ziara yake ya siku tano Kisiwani Pemba siku ya Jumaamosi tarehe 21 kwa kufanya majumuisho ya ziara yake katika Mkoa wa Kusini Pemba huko Wesha katika Hoteli ya Misali Sun Set na baadae kurejea Unguja.

Wakati huo Kamati ya Kitaifa ya zao la Karafauu ilikutana leo huko katika ukumbi wa Makonyo Wawi Chake Chake Pemba chini ya Mwenyekiti wake Waziri wa Biashara , Viwanda na Masoko Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui ambapo kikao hicho kilitathmini uvunaji na ununuzi wa Karafuu na kuridhika nao.


IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.