Na Thabit Jaha, Zanzibar.
Chama cha Mapinduzi(CCM) kimesema Muungano hautavunjwa na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu kwani Jumuiya hiyo haina mamlaka ya kuwaamulia Watanzania hatma na mustakabali wao.
Onyo hilo limetolewa na Jumuiya tatu za CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa mabata Zanzibar ambapo iliweka bayana msimamo wa Chama hicho kulinda Muungano na Mapinduzi kwa gharama yoyote.
“Sisi tunawaambia Muungano hautavunjika kwa kisingizio cha katiba mpya,katiba mpya ni sehemu tu ya mabadiliko ya kukuza demokrasia ya utawala…CCM ikiwa zao la ASP na TANU tunawajibu wa kutetea historia yetu ya umoja na mshikamano” Alisema Mjumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Wazazi Taifa, Ramadhan Abdallah Ali
Alisema kumejitokeza kikundi cha watu wanaojificha kwenye mwamvuli wa Jumuiya ya kidini kuandesha kampeni chafu za kusambaratisha Taifa la Tanzania kwa kutumia mpango mkakati wa kutoa elimu ya uraia Visiwani Zanzibar na kushangazwa na vyombo vya Dola kuwafumbia macho watu hao.
“Vyombo vya Dola vinakaa kimya,viongozi wa Kitaifa wanatukanwa na kudhalilishwa na kikundi hichi, haiwezekani watu wanachochea uasi dhidi ya Jamhuri,lakini hakuna hatua zinazochukuliwa…CCM tunasema muda wa kuwavumilia umekwisha” Alionya Mjumbe huyo.
Alisema kwamba wanaopinga na kutaka kuvunja Muungano wa Tanzania pia wana lengo na mipango maalum ya kusambaratisha Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964 ambayo yaliongozwa na ASP .
“Kwa kweli tusifanye mchezo na uchochezi unaofanywa na watu hao, vikundi kama hivi ndio vilianzisha vurugu katika Mataifa mbalimbali,leo mnasikia kuna Al shabab,Boko- haram,Fisi na wengineo wote hao kabla walijificha kwenye mwamvuli wa dini,hawa wa Zanzibar tumashawabaini, tuwakatae” Alisisitiza.
Mkutano huo umefanyika huku kukiwa na kundi lililoanzisha kampeni ya hadharani kushawishi wananchi kukataa Muungano kwa madai kwamba haujaleta faida kwa Wazanzibari.
Mbali na udini, pia kikundi hicho haikijitofautisha na vyama hasimu vilivyokuwa vikipinga Muungano ambapo matamshi yao, vitendo na muenekano wao hauna tofauti na wapinga mapinduzi.
Katibu huyo mstaafu wa CCM Mkoa Mjini Magharibi amesisitiza kuwa Mapinduzi ya 1964 ndiyo yaliowaletea heshima na kutambuliwa kwa utu wao waafrika wanyonge waliokuwa wakibaguliwa na kutumikishwa.
“Hakuna mjinga yeyote hapa Zanzibar asiejua kuwa mpango wao si kueneza dini ila ni kutaka kusambaratisha Mapinduzi,wao wanaelewa fika kuwa Muungano huu hautavunjika milele kwasababu hawakuunda wao na wala hawatambui madhumuni ya nchi mbili hizi kuunganishwa ”Alisema Ali
Ali aliwakumbusha wananchi utawala wa Kifalme wa Oman waliikalia Zanzibar kwa miaka 132 kwa kulindwa na Uingereza wakichota rasilimali ,kuwatumikisha na kuwabagua wananchi bila ya kufanyika kura ya maoni ili kujua wananchi wangapi wanautaka ukoloni au wanaupinga.
Alitoa mfano kuwa tangu kufuzu kwa Mapinduzi,Mfalme na aila yake, wapinga mapinduzi walijaribu kutaka kuyaondoa mapinduzi ambapo jaribio kubwa ni lile la kumuua Rais wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,marehemu Abeid Amani Karume.
Alisema wana CCM na wazalendo wengine hususan wanyonge wa Zanzibar wanajua kuwa wale waliopinduliwa hawakupenda kuondoshwa na hadi sasa bado wanaota na kutamani kurejea kushika utawala.
“Uamsho msijifiche nyuma ya kivuli cha dini,uislam ni dini adhim na tukufu,hakuna hata dini yoyote inayoelezea uvunjifu wa amani kwa kuchochea utengano miongoni mwa jamii, acheni kujifanya mnaeneza dini wakati mnafanya siasa” Alionya.
Akizundua Tume ya Katiba,Rais Jakaya Kikwete alisisitiza kwamba katiba mpya haitavunja Muungano na kuwaonya watu wanaochochea suala hilo kuacha mara moja.
wa Zanzibari karibuni wote tuko pamoja na muamsho katika harakati za kuikomboa nchi yetu kutoka katika utawala wa mkoloni mweusi,
ReplyDeleteNyie wana maskani wa ccm kama hamuuna uzalendo na zanzibar wafuateni wenzenu wa Tanganyika huko
na wambiieni wakubatizeni kabisa, malimbukeni wakubwa nyie....nyie ni wavamizi tu wa nchi yetu baba yenu nyerere alikuleteni hapa baada ya mapinduzi kuja kuitawala zanzibar....lakini siku zenu zimebaki kidogo sana za kuishi zanzibar...hilo mulijue
This comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteVibara wakubwa wa Kidanganyika nyie...munazania muna miliki hii nchi yetu tuwewauzia nyinyi au vipi?
ReplyDeleteHakuna ASP/CCM au chama chochote kile kinachomiliki hii nchi..Hii ni nchi ya Wa Zanzibari na itaendelea kuwa nchi yao mpaka mwisho wa dunia hii Raia ndio mwenye uamuzi na nchi yao, kama hamutaki kutusikiliza raia basi tuuweni sote halafu muletee wa tanganyika zaidi muje muishi nao
lakini mujue kuwa kuna wa Zanzibari zaidi ya laki tatu wanaishi nje ya Zanzibar lazima waje kulipiza kisasi kwa ajili ya Familia zao.
Mimi ninahisi kwamba Mheshimiwa Ramadhan Abdallah Ali hajayaelewa yale wanayoyasema Uamsho na anajaribu kutuletea ukereketwa. Kama sijakosea Uamsho inajaribu kutufahamisha Wazanzibari jinsi ya kuitumia haki yetu na kuamua ni Muungano wa aina gani Wazanzibari tunautaka na ambao utaleta faida na maendeleo ya visiwa vyetu.
ReplyDeleteWewe mwanamapinduzi Mheshimiwa Ramadhan Abdallah Ali tafadhali wasikilize wahubiri wa Muamsho yale wanayosema na sio ukurupuke na Umapinduzi wako tuu. Jee sio hao hao Muamsho wanaoitetea Jamhuri ya watu wa Zanzibar na Jamhuri ya watu wa Zanzibar ilikujaje? Si ililetwa na hayo mapinduzi? Hivyo usijaribu kuwapotosha Wazanzibari ambao wanaitetea nchi yao ambayo ni Jamhuri!!!
mm pia nina wasiwasi na huyu mapara mbona wanayosema jumuiya ya uamsho hutuekei hapa tukaona yote.ila kwa sababu ya ukereketwa wake yaliyosemwa na ccm ndo anatuwekea hapa.weka yote ww muandishi wa hbr ufunguke akili.co mnakaa na kudanganywa wa2 wanataka kupindua mambo ya zamani.vunjen hoja za uamsho ndo mlete nyengne.ss huyo kiongozi kuamrisha polisi kupiga wa2 co kuvunja amani.hao hao mtawafanya wajinga.siku zenu zimefika mwisho na km mtatuua tueni sote.
ReplyDeleteBila shaka UAMSHO hawana ubavu wa kuvunja muungano ila wanachofanya ni kuwaelimisha Wanzibar juu ya udhalimu wa muungano huu walikuwa nao na tanganyika, hivyo ni juu ya Waznzibar wenye kuelewa lengo la UAMSHO ni kuelisha na kuwaamsha Wazanzibar wachache waliorogwa na CCM pamoja na CUF.
ReplyDeleteKuhusu Mapara, jamani usiwe na wasi2 huyu ni Mtanganyika sasa unadhani ataandika au kuwashabikia UAMSHO?
Ramadhan Abdallah Ali au ccm zanzibar sasa wanatapata maana wanaona they days are number now lete hoja za kuwa muungano huu upo na sio kushambulia jumiya ya uamsho tunasema jamhuri y watu wa zanzibar kwanza baadae ndiyo hivyo vyama vyenu vya siasa.
ReplyDeleteMimi, naskitishwa sana na SMZ kuwaachia hawa wahuni(UWAMSHO) watuharibie nchi yetu.
ReplyDeleteBinafsi, nna wasi wasi baadhi ya viongozi wa SMZ wanawaunga mkono lkn. wakumbuke UWAMSHO wakifanikiwa kuwadanganya w'chi na wao hawatobaki!
Yaani serikali inawaachia uwamsho wanapandikiza chuki za kidini ,kikabila pamoja asili za watu, halafu wanadai eti hawawezi kuwadhibiti? wakati tuliyaona yaliyowafika CUF (1995-2005)!
Miaka takriban 40 Waz'bari tunasoma bure kuanzia std.1 hadi chuo kikuu, hivi kweli hii ndio elimu tuliyoipata ya kutukana na kubagua watu?
Hivi wakati mnazungumzia wabara waliopo visiwani mnaangalia pia wazenji waliopo bara na mafanikio yao? au ndio yale ya mwenye chuki ni kipofu haoni?
Jamani tukianza kubaguana hapa hatobaki mtu kwani hata huyo FARIDI tutamrejesha "HADHRA'MUT" akashughulikie matatizo yao!
Kama unajiona ni mzawa, ukumbuke kwenu ni shamba kwenu au nyumbani kwako!
@Adhubany, wewe unawaita Uamsho wahuni, unwajua uamsho ni kina nani? mna masheikh ndani yao pamoja na viongozi wa jumuia ya Maimam Zanzibar , jee unaweza kutueleza ni uhuni gani wanaofanya? la pili umuzungumza kuhusu ubaguzi, unauliza jee ni wazanzibari wangapi walioko bara! jawabu ni Wazanzibari wengi tu wako bara lakini Wazanzibari popote waliopo hawachafuwi culture ya wazalendo bali wanaelimisha maadili mazuri wala hawawaingilii juu ya uongozi wenu wala mipangilio yenu ya nchi, hiyo ndio sifa ya Mzanzibari, sasa kwa jamaa zako wa tanganyika ni kinyume na hayo , naweza kusema kuwa zaidi ya asilimia 75 ya Watanganyika wanaokuja Zanzibar hivi sasa wanakuja kwa nia ya uharibifu , tafauti na waliokuwa wakija zamani wao ilikuwa ni jembe tu.
DeleteKwa kumalizia Zanzibar ni ya Wazanzibari na Uamsho pia ni wazanzibari wataendelea kuamsha watu hata kama hampendi, hakuna ilani ya chama walailani ya serikali. ZANZIBAR KWANZA ufurukutwa baadae.
Na mimi ntaanzisha Jumuiya yangu ya Kuwalisha watu chuki na ubaguzi, maana naona kila mtu ana NGO yake ya kujipatia ugali.
ReplyDeletewewe unaweza kuanzisha Jumuiya, kwani hujui kama JUMUIYA NI BIASHARA? ila kuna haja kubwa ya kuangalia kwa undani wanachokipigania UAMSHO! Hawa ni watu wa dini na wameanzisha Jumuiya zao kwa maslahi ya dini wala sio Biashara. Kwa hivyo, hata wakisema leo, watu wale bata, basi ujue dini yao ya Uislamu inawaruhusu na inawahimiza kufanya hivyo. Uamsho kwa vyovyote ilivyo, wanapigania Dini yao ya Uislamu ndani ya Zanzibar. Na wanakerwa sana kuona dini yao inadhalilika na zaidi inadhalilishwa makusudi. Sasa kuna sababu nyingi za kudhalilishwa ama kuharibiwa kwa dini hiyo, moja kubwa (KWA MUONO WAO) ni huu Mfumo wa Muungano! Hivyo, mimi nawafahamu kwamba, sio kama wanapinga Muungano, ila hawapendi ZANZIBAR na zaidi UISLAMU wao kudhalilishwa kwa kisingizio cha Muungano na zaidi kwa mfumo wa Muungano uliopo!
ReplyDeleteAisee, watu wengine kumbe bado wana utomvvu wa macho, na mnukuu huyu katibu wa Catholic Charch Movement (CCM) ANASEMA "wanaelewa fika kuwa Muungano huu hautavunjika milele kwasababu hawakuunda wao"
ReplyDeleteNapenda kumfahamisha aache ujinga, isiwe dunia haitabaki milele, iwe Muungano? halafu anasema hautavunjika kwa sababu Uamsho hawakuunda wao, kwani unadhani huu kaunda mama yako?
Tunasema wazanzibari sote wenye akili, tusio machizi kama wewe, tuko pamoja na Uamsho, tuko tayari kufa kwa kuitetea nchi yetu. Nyinyi mnafata mawazo ya makafiri kuidhulumu zanzibar, lakini mwisho wa hayo umefika.
A.alaykum -mimi napenda niongezee kuwakumbusha kwamba uhusiano wa kujamii wa wazanzibar na watanganyika upo miaka mingi kabla ya muungano lakini huu wa serikali moja na udhalimu unaofanyika dhidi ya Zanzibar ndio tumechoooooooooooooooooooooooooooooooooka taaabani hali zetu tuacheni tupumuwe japo miaka kumi then tutafikiria kama tutaka tena hayo maungano kwa kutumia muda huo mtajifunza mengi kutoka znz.
ReplyDelete