Habari za Punde

Wafanyabiashara wa Vinyago Walalamikia Kukatishwa Leseni Mara Mbili

Na Mwanajuma Mmanga

WAFANYABIASHARA wanaouza zawadi za kitalii katika maeneo ya Mji Mkongwe wamelalamikia tatizo la kukatishwa leseni mara mbili kati ya Manispaa na Kamisheni Utalii Zanzibar.

Wafanyabiashara hao wametoa malalamiko hayo hivi karibuni kufuatia operesheni maalum iliyofanywa na Kamisheni ya utalii katika kuwasaka wanaokwepa kukata leseni katika maduka mbali mbali ya mji Mkongwe, Zanzibar.

Wafanyabiashara hao walisema hawajakaidi kukata leseni bali walikata leseni Manispaa wakati walitakiwa kukata leseni hizo Kamisheni ya Utalii.

Walisema walishangazwa na kitendo cha Kamisheni ya utalii kuwafungia maduka wakati wao walijua leseni hizo zinatakiwa kukatwa Kamisheni ya utalii.

Hata hivyo, baadae wafanyabiashara hao walikata leseni mpya Kamisheni ya Utalii na kuzitaka pande hizo mbili kukaa na kuamua wapi hasa wafanyabiashara haop wakate leseni ili kuepuka kusumbuliwana upande mmoja wapo kati ya Manispaa na Kamisheni ya utalii.

Katika kutembelea Zanzibar Leo imeshuhudia baadhi ya wafanyabiashara hao tayari wameshakata leseni zao kwa mwaka 2012 katika Kamisheni uya utalii.

Nae Mkuu wa Kitengo cha Doria wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Ramadhan Mohammed, Rifai alisema pamoja na wafanyabiashara hao kukata leseni kutoka Kamisheni yake lakini hawazitambui kwa kuwa hazina uthibitisho.

Hata hivyo, Wafanyabiashara hao walisisitiza kwamba leseni hizo wamekata Kamisheni ya utalii lakini kauli zao zinapingana na zile za Kamisheni ambapo inasisitiza wafanyabiashara hao hawakukata leseni kwenye Kamisheni hiyo.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.