Madereva wakiwa katika mabishano ya kila mtu akimtaka mweziwe arudishe gari nyuma ili apate kupita katika eneo la barabara ya shangini vuga korti, na kusababisha msongamano wa magari katika barabara hiyo na kuleta usumbufu wa watu wanaotembea kwa miguu nac wenye vyombo vya moto.
Ilichukuwa muda hadi kukubaliana kwa baadhi ya madereva wa gari nyengine kuwaomba kuwacha ubishi huo.
Watembea kwa miguu wakikatisha magari yaliokuwa katika msongamano huo na kuwa bughudha kwao. mvutano huo umechukuwa kama dakika 20 za kubishana na hatimai kupata suluhu, baada ya kuwa na msongamano mkubwa hadi kufika maeneo ya Mahakamani na kwa upande wa pili kufika posta.
No comments:
Post a Comment