Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imeendelea na jitihada zake za kuhakikisha ushiriki wa makundi maalum katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, kwa kutoa mafunzo maalum ya namna ya kutumia karatasi za kupigia kura kwa mfumo wa kugusa na kutambua kwa vidole, maarufu kama Nukta Nundu (Tactile).
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Kamishna wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Mhe.Idrissa Haji Jecha , alisema kuwa hatua hiyo inalenga kuhakikisha watu wenye ulemavu wa kuona wanatumia haki yao ya kikatiba kwa uhuru na bila utegemezi kwa wengine.
“Changamoto inayowakabili ndugu zetu hawa imekuwa ni utegemezi kwa watu wengine kuwasaidia kupiga kura, jambo ambalo linapunguza faragha na uhuru wao wa kuchagua viongozi wanaowataka,” alisema.
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar tayari imeshatengeneza kifaa maalum kwaajili ya watu wasioona (tactile ballot folder) na imeanza kutoa mafunzo kuhusu namna ya kutumia kifaa hicho.
Aidha, washiriki wa mafunzo hayo wamehimizwa kuwa mabalozi wazuri katika jamii zao kwa kuwafundisha wenzao ambao hawakupata fursa ya kushiriki mafunzo hayo ili nao waweze kutumia haki yao ipasavyo.
“Tume inajivunia kuwa na nyinyi katika safari ya kuimarisha usawa, heshima na haki kwa kila raia wa nchi yetu,” alisema Kamishna Idrissa.










No comments:
Post a Comment