Habari za Punde

Ofisi ya Rais na BLM Washiriki Usafi Forodhani

Habari Maelezo Zanzibar 5/5/2011 

 Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi leo wameshiriki katika kazi za usafishaji wa mji katika eneo la Forodhani Mjini Zanzibar. 

 Utaratibu huo ni uzinduzi wa kazi za Usafi unaoongozwa na Baraza la Manispaa hapa Zanzibar ikiwa ni sehemu ya mikakati yake yakushajiisha Wananchi juu ya Usafi katika sehemu za Mjini na Nyenginezo. 

Akielezea juu ya uzinduzi wa Usafi huo, Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Zanzibar Rashid Ali amesema kuwa Kazi hiyo ya usafi kwa sehemu za Mjini na nyengineze itakuwa ikifanyika kila mwanzoni mwa mwezi kwa siku ya Jumaamosi. 


 Amesema kuwa kazi hiyo itakuwa endelevu na sio ya zima moto na Jumaamosi ijayo itakuwa kwa kila Nyumba ,Wadi na Shehia kufanya usafi na wao watakuwa na Wajibu wakukusanya Taka hizo ili wazipeleke kunakohusika kwa kuzitupa.

 Aliendelea kusema kuwa Jumaamosi nyengine kazi hiyo itaendelea tena hiyo ambapo watalazimika kufunga baadhi ya Nija kuanzia saa12 asubuhi hadi saa 3 asubuhi. 

Nae Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mwinyiussi Abdulla kwa niaba ya Waziri Dkt Mwinyihaji Makame amesema kuwa Madhumunui ya Ofisi hiyo kuanzisha utaratibu huo wa kufanya usafi kila siku ya Jumaamosi ya wanzoni mwa mwezi ni kuwashajiisha Wananchi kuona kuwa kazi hiyo si ya Baraza la Manispaa tu bali ni ya kila mtu. 

Alisema kuwa ni wajibu wa kila mtu pale alipo kuungana na Serikali katika kazi hiyo ya kufanya usafi kwani ni kwa faida ya mtu mwenyewe na Taifa kwa ujumla, Katika uzinduzi huo Maofisa mbali mabli katika ofisi hiyo walishiriki katika kazi za usafi wakiwamo Manaibu Makatibu Wakuu, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Masheha pamoja na Wafanyakazi kutoka Taasisi mbali mbali ziliomo katika Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. 

 IMETOLEWA NA IDARA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.