Habari za Punde

Wakulima 500 wa Kilimo cha Mpunga Bonde la Ukele Warejea.


Na Haji Nassor, Pemba

ZAIDI wa wakulima 500 wa kilimo cha mpunga ,wameanza kurejea kwenye bonde lao Ukele Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, baada ya kulihama kwa muda mrefu kwa kuingia maji chumvi , na sasa kujengwa tuta la kuzuia maji hayo na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF).

Aakizungumza na waandishi wa habari kwenye ziara maalum ilioandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari (PPC), ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani, Mkuu wa Idara ya Umwagiliajia maji Pemba, Mbarouk Ali Mgau, alismea idadi hiyo ndio waliokuwa wamelihama bonde hilo.


Alisema kuwa ujenzi wa tuta hilo la kuzuia maji ya chumvi, limewakombo wakulima hao na sasa wamerejea wakiwa na matumaini makubwa, kutokana na kuwa na uhakika wa kutovamiwa na maji kama ilivyo kuwa awali.

Mgau alieleza kuwa jumla ya shilingi 230 milion ndizo zilizotumika katika ujenzi huo wa tuta hilo, ambapo kati ya fedha hizo shilingi 88 milion, zilitolewa na TASAF na shilingi 121 milion zilitolewa na Serikali kuu .

Alieleza kuwa chanzo ya ujenzi wa tuta hilo, ulitokana na wakulima wenyewe wa shehia tatu za Micheweni, kumuelezea Rais wa Zanzibar juu ya tatizo lao hilo na juhudi za haraka zikachukuliwa na Serikali na washirika wake hao na hadi mwanzoni mwa mwaka huu ujenzi wa tuta hilo ukakamilikia kwa hatua za awali.

''Wakulima wenyewe ndio waliokuja na wazo hilo kuanzia ngazi ya Idara hadi Serikali kuu na Rais wetu akalikubali wazo la kujenga tuta hilo lenye utefu wa mita 700 , na leo hii wakulima hawana hofu ya kuvamiwa na maji chumvu'',alizidi kufafanua Mgau.

Aidha Mkuu huyo wa Idara ya Umwagiliaji, alisema kwa sasa bonde hilo la Ukele halimo kwenye programu za kuweka mindombinu ya umwagiliaji, lakini wanatarajia wazo hilo kulifikisha Serikali kuu .

Nae Mkulima Hadia Mwinyi Suwed alisema kuwa, kero kubwa maara baada ya kumalizika kwa ujenzi wa tuta hilo kwa hatuza awali, ni baadhi ya wafugaji kupitisha mifugo yao juuu ya tuta hilo .

''Wafugaji bado hawajatufahamu na tunaendelea kupambana nao maana wapo wachache wasugu'',alieleza Mkulima huyo.
Katika hatua nyengine alisema miongoni mwa sababu iliowafanya walikimbie bonde hilo kwa muda mrefu kutokana na kuingia maji ya bahari, ni pamoja na kukithiri kwa ukataji wa mikoko (mikandaa) kwa ajili ya kuni na ujenzi.

Nae Hamad Omar Ibrahim, alisema wanatarajia kipato chao cha mpunga kuongezeka kutokana na maji ya chumvi ambayo yalikua adui wa zao la mpunga kudhibitiwa kwa ujenzi wa tuta hilo.

Hata hivyo amewaomba wakulima wenzake kuhakikisha wanayafuata kikamilifu maelekezo ya wataalamu wa Idara za misitu na Mazingira, ili kuona kuwa tuta hilo linadumu kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na upandaji wa miti pembezoni mwa tuta hilo.

Kwa upande wake Aifisa Mipango Wilaya ya Micheweni Hamad Massoud Hamad, alisema kuwa Serikali ya Wilaya, imefarajika kuona idadi kubwa ya wakulima kurejea kwenye bonde hilo ambalo kwa kiasi kikubwa litapunguza uhaba wa chakula Wilayani humo.

Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, eneo lake kubwa limejengeka kwa mawe na kusababisha wakaazi wa eneo hilo kukumbwa na kiangazi kizito kinachooambatana na uhaba wa chakula kila baada ya muda mfupi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.