Na Mwantanga Ame
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Zanzibar, Said Ali Mbarouk, amesema licha ya kujitokeza kwa mivutano ya vurugu Zanzibar, bado usalama wa watalii upo katika hali nzuri na waendelee kuja kwani kinachotokea ni vuguvugu za kutanuka kwa demokrasia.
Waziri huyo aliyasema hayo jana alipozungumza na Viongozi wa Jumuiya za Utalii wanaoshughulikia usafirishaji na Wawekezaji katika sekta hiyo, ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar.
Waziri huyo alisema sekta ya utalii licha ya kujitokeza vurugu zinazoendelea sasa bado iko salama kwani kinachotokea ni Changamoto za vugugu za mabadiliko ya demokrasia ambayo mataifa yote duniani hukumbwa na hali hiyo.
Alisema yapo mataifa kadhaa duniani hivi sasa yanakabiliwa na hali za mivutano ya watu katika kudai haki zao ambayo hutumia njia tofauti, jambo ambalo huondoka baada ya muda mfupi na sio vitu vinavyoendelea kwa vile tayari serikali ina mipango kadhaa ya kukabiliana nayo ili kurudisha amani ya nchi.
Kutokana na hali hiyo Waziri huyo alisema kinachotokea hivi sasa kisiwe kinatumika kuuwa sekta ya utalii kwani serikali kwa nguvu zote itahakikisha amani ya nchi inarudi kama kawaida na usalama wa kila raia wakiwemo wageni unalindwa.
Alisema Serikali ya Zanzibar mara kadhaa imekuwa ikieleza juu ya suala la kulinda wageni na itahakikisha hilo linafanyika katika msimu ujao wa watalii ili kuona sekta hiyo inakuwa yenye tija kwa taifa.
Akiendelea Waziri huyo alisema hivi sasa serikali inajiandaa kupokea watalii wapatao 300,000 katika msimu ujao unaotarajiwa kuanza baada ya wiki tano zijazo, jambo ambalo linahitaji kuona kwa kila hali nchi inabakia katika amani ya nchi.
Waziri huyo aliwataka viongozi wa Wawakilishi wa mataifa mbali mbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa Zanzibar na Mashirika ya Kimaitaifa na ya Ndege kuwafikishia ujumbe huo na serikali inaahidi kuwapa usalama wa hali ya juu watalii wote wataoingia nchini.
Nao baadhi ya wawakilishi wa Nchi mbali mbalina mashirika ya Uwekezaji wameiomba serikali kuendelea kujenga mshikamano kuimarisha sekta hiyo na watakuwa tayari kuona ujumbe huo wa serikali wanaufikisha katika sehemu zao.
Aidha walipongeza hatua ya Serikali, pamoja na jeshi la Polisi kwa namna walivyolishughulikia suala la machafuko hayo kwa muda mfupi na kwa njia bora.
Kwa viongozi wa namna hii Z'bar itaendelea kubaki nyuma kwa miaka mingi ijayo..ovyo kabisa!
ReplyDeleteMnaacha makundi yenye uhusiano na Al-qaeda kutufanyia vurugu ili wazungu wasije mtuuwe njaa kwa vile nyie mnashiba na familia zenu.
Eti changamoto za mabadilikiko ya kidemokrasia..shame on you!.. haya waacheni basi wende na ikulu si ndio nchi nyingine wanavyofanya
Mimi nlidhani atasema serikali imejipanga kutumia 'resources' zake zote ku'counter' upotoshaji wa habari ktk mitandao ya nje pamoja na ile ya Bara na kuandikia balozi mbali mbali na kuzipa hakikisho.
Kwa maelezo haya ni wazi kwamba CUF wapo nyuma ya hawa vijana..eti kutanuka kwa demokrasia!..kama mnaamini demokrasia haijatanuka kwanini msiseme Bungeni na kwenye Baraza lawawakilishi..na nyinyi mpo?