Afisa Muandamizi Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar Seif Suleiman, akitowa maelezo kwa Wananchi waliofika katika viwanja vya maonesho jinsi Benki ya Watu wa Zanzibar inavyotowa huduma za Kibenki kwa Wananchi, akiwa katika viwanja vya maonesho Mjini Dar-es-Salaam.
Mjasiriamali kutoka Kisiwani Pemba Chakechake Bahati Kawambwa, akitowa maelezo ya bidhaa zake za mafuta ya Nazi na mengineo wakati wa maonesho hayo ya Wajasiriamali.
Mjasiriamali kutoka Chakechake Pemba akifanya biashara ya bidhaa mbalimbali katika maonesho ya Kuwawezesha Wajasiriamali Kibiashara, maonesho hayo yamewashirikisha Wajasiriamali wa Mikoa yote ya Tanzania na Zanzibar.
Mjasiriamali kutoa Mjini Zanzibar akiwa katika banda lake akitangaza biashara yake wakati wa maonesho ya Wajasiriali yanaofanyika viwanja vya Mnazimmoja Mjini Dar-es-Salaam.
Mambo ya Zenj hayo katika Viwanja vya Maonesho ya Wajasiriamali , Mjasiriamali akitowa huduma ya Urojo kwa Wananchi wanaotembelea banda la Zanzibar kuangalia bidhaaa mbali mbali.
Mjasiriamali kutoka Mkoani Kigoma Charles, akionesha bidhaa zake zitokanazo na Mtii wa Karakanda, ukiwa umetengenezwa bidhaa mbalimbali za aina ya Chupa ya Chai, HotPort, akiwa katika viwanja vya maonesho. ( unaweza kumpata kwa namba hii 0717 968825.
Mjasiriamali wa kufuma Masuweta akiwa katika kazi hiyo katika viwanja vya Maonesho Mnazi Mmoja wakati wa maonesho hayo.
No comments:
Post a Comment