Habari za Punde

Polisi Arusha yashikilia 12 ikiwahusisha na ujambazi

Joseph Ngilishoi, ARUSHA
JESHI la polisi mkoani Arusha linawashikilia watu 12, likiwahusisha na matukio mbalimbali ya uhalifu wakiwemo kupora mamilioni ya fedha katika ofisi ya Askofu wa kanisa la Anglikana, Stanley Hotay.

Kamanda wa polisi mkoani hapa, ACP Liberatus Sabas alisema kuwa kukamatwa kwa wahalifu hao kunatona na jeshi hilo kufanya msako mkali uliofanikisha kukamatwa watuhumiwa hao wa uhalifu.

Sabas alisema kuwa, wahalifu hao wamekuwa wakifanya uhalifu ukiwemo uporaji, unyang’anyi wa kutumia silaha na matukio mbalimbali, ambapo jeshi la polisi baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema.

Aliwataja baadhi ya washukiwa hao wa ujambazi ni pamoja na Abdy Shaban (22) mkazi wa Bonite mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro ambaye ni kati ya watatu walihusika na uporaji katika ofisi ya Askofu Stanley Hotay.

Taatifa zinaeleza kuwa Askofu huto aliporwa kiasi cha shilingi milioni 9, huku polisi ikiendelea kuwasaka watuhumiwa wengine wawili waliohusika na tukio hilo.

Wengine wanaoshikiliwa ni Richard Andrew (28) mkazi wa Unga Ltd, Inocent Lyimo (34) mkazi wa kambi ya fisi, Wilson Edward (38), mkazi wa kambi ya fisi, William Robert (33) kambi ya fisi, Inocent Julius (29) mkazi wa unga Ltd na Mohamed Abdu (26) mkazi wa Ngarenaro.

Wengine ni Ismail Bakari (31) mkazi wa Esso, Hussein Kibwana (28) mkazi wa Ngarenaro, Yasin Athuman (34) makao mapya na Saitoti Stanbul (23) mkazi wa Sakina mjini hapa.

Aliongeza kuwa, watu hao walikuwa wakitafutwa muda mrefu sana na rekodi za  jeshi la polisi zinaonyesha kuwa wamekuwa wakihusika kujirudia na matukio hayo ya uporaji jijini Arusha na nje ya mkoa wa Arusha.

Kamanda Sabasi alisema upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.