Na Mwantanga Ame
HUKU wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakijadili bajeti ya mwaka wa fedha wa 2012/2013, kilio cha kero za Muungano kimetawala na kutikisa michango ya wajumbe wa Baraza hilo.
Wajumbe hao walisema kuwa kero za Muungano zimekuwa kero kubwa kwa uchumi wa Zanzibar na kwamba zinahitaji kurekebishwa hivi sasa badala ya kusubiri mchakato wa katiba mpya.
Akichangia bajeti hiyo, Mwenyekiti wa kamati ya Wenyeviti wa Baraza la Wawakilishi, Hamza Hassan Juma (Kwamtipura), alisema kuwa serikali inapaswa kuja na majibu mazuri juu ya namna ya kero za Muungano zitakavyomalizwa, kwani zinakandamiza uchumi wa Zanzibar.
Hamza alisema inasikitisha kuona serikali ya Muungano hivi sasa imekuwa na mambo mbali mbali ya serikali inayotakiwa kuyafanyia kazi lakini hakuna lililofanyika wakati serikali ya Muungano ikiwa inatekeleza vyema matakwa yake.
Mwenyekiti huyo alisema serikali ya Zanzibar inakosa majibu juu ya suala la mgao wa Muungano wa asilimia 4.5 ambao kwa muda mrefu yametolewa mapendekezo ya asilimia 11.5 lakini BOT bado halijatekelezeka hadi sasa.
Alisema jambo linaloshangaza kuona baada ya kupelekwa mapendekezo hayo serikali ya Muungano imeipatia gawio la asilimia 7.8 huku kukiwa hakuna muendelezo wa hatma ya suala hilo.
Alisema kuwapo kwa gawio hilo limeifanya serikali ya Zanzibar wakati ikisubiri suala hilo kumalizwa katika vikao vya kero za Muungano imekuwa ikikosa shilingi bilioni 7,000,000,000 kati ya shilingi bilioni 15, ambazo zilitakiwa kuingia katika mfuko wa hazina ya Zanzibar kama hilo lingekuwa limemalizwa.
Suali jengine linaloonesha kutokuwepo kwa utayari wa serikali ya Muungano kulifanyia kazi kwa haraka, ni kodi ya mishahara ya wafanyakazi wa Muungano ambao wanafanya kazi hapa Zanzibar ambapo inakosa shilingi bilioni 18.
Alisema kama mambo hayo yangeliweza kutolewa maamuzi ya haraka, kwa kiasi kikubwa zingeweza kuisaidia serikali ya Zanzibar kupata gawio lake kwa miaka mingi badala ya hivi sasa kuendelea kutolewa kwa fedha hizo kama ni huruma.
Aidha alisema kero pia ziko katika suala la elimu ya Juu ambapo serikali ya Zanzibar itapaswa kuona inadai serikali ya Muungano kwa mwaka ujao wa fedha kupatiwa asilimia ya gawio la Zanzibar ikiwa ni hatua itayoweza kujipanga vyema katika kutoa elimu ya juu.
Mwenyekiti huyo, aliikosoa bajeti hiyo, kwa kueleza kuwa kodi ya umeme ambapo alisema inaweza ikachangia kuongeza gharama za maisha kwa wananchi na kuiomba serikali kuiondoa hadi kamati ya Baraza la Wawakilishi litapomaliza kufanya uchunguzi wake katika shirika la Umeme.
Kutokana na hali hiyo Mwenyekiti huyo aliishauri serikali kufikiria kuwaangalia watendaji wake kwa kuhakikisha wanawatumikia wananchi huku serikali ikawachukulia hatua za kinidhamu wanaotajwa kuibia serikali.
Aidha, Mwenyekiti huyo pia alieleza dhamira ya Kamati hiyo kutaka kuwasilisha maombi ya kuifanyia uchunguzi Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) baada ya kujionesha baadhi ya Watendaji katika kitengo cha Bandarini kuonekana kujihusisha na uvujaji wa mapato.
Eneo jengine ambalo kamati hiyo imetishia kuizuia bajeti hiyo ni juu ya suala la ajira kwa vijana kutokana na hivi sasa kuwepo kwa taarifa za wageni kuajiriwa kwa wingi katika mahoteli ya kitalii huku Wazanzibari wakikoseshwa nafasi hizo.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Uzini (CCM), Mohammed Raza alisema uchumi wa Zanzibar unaweza ukakosa kunawiri ikiwa baadhi ya mambo yakiachiwa moja kwa moja kutekelezwa na serikali ya Muungano likiwemo suala la kujiunga na taasisi ya kimataifa ya Kiislamu (OIC).
Aidha Mwakilishi huyo alihoji juu ya suala la Afrika Mashariki nalo linahitaji kuangaliwa katika haki ambazo itaweza kuzipata kama Zanzibar bila ya kuingia kama ipo chini ya mwamvuli wa Tanzania.
Naye Mwakilishi wa Kitope Makame Mshimba Mbarouk alisema serikali itapaswa kujiangalia katika miradi ya uwekezaji kutokana na baadhi ya wawekezaji kufutiwa miradi yao ikiwa analipia gharama kubwa na kupewa watu wanaolipiwa kiasi kidogo cha fedha.
Alisema hivi sasa kuna watu wamekuwa wakiondolewa kwa chuki katika baadhi ya miradi hiyo jambo ambalo linapoteza imani ya wawekezeji kuwekeza Zanzibar na kuahidi kuizuiya bajeti hiyo hadi atapopewa maelezo ya kija juu ya suala hilo.
Nae Mwakilishi wa Chonga (CUF), Abdalla Juma Abdalla, aliiomba serikali kuona inatekeleza vyema bajeti hiyo na kuahidi kuwa hatoacha kuiziya hadi atapopewa maelezo ya kina kutokana na kujitokeza mambo mbali mbali katika serikali.
Mwakilishi wa Ziwani, Rashid Seif, akitoa mchango wake aliitaka serikali kuona inajipanga vyema katika suala la kusimamia sekta ya elimu kutoka an akuanza kuonekana eneo hilo huenda kukawa na wajanja wanaotumia vibaya nafasi zao.
Hongereni sana wawakilishi kwa michango yenu makini, mimi naamini kama mna nia ya dhati juu ya hayo mnayoyasema, hakuna lisilowezekana.
ReplyDeleteTungependelea pia tusikie maoni ya wale tuliochaguliwa wajumbe wa kamati ya kumaliza kero za muungano hapo barazani.
Aidha kama nia ya dhati ipo tungeomba tuanze na yale yaliyo ktk uwezo wetu kama vile uchunguzi wa haraka kwa mashirika yetu kama vile ZRB na ZECO.. huko kunatisha!
Ama kuhusu suala la wageni kuajiriwa ktk sekta ya utalii mimi nailaumu zaidi SMZ kwa kusindwa kuwajenga watoto kisaikolojia na kuamini kua utalii ni ajira kama zilivyo nyingine!
Wenzetu unamkuta mtu na Degree lkn anakuja kutafuta kazi ya htl Z'bar wakati hapa kwetu ndio kwanza tunakumbuka shuka!..wengi tulikua na 'nagative attitude' na utalii tusione leo maji yashazidi unga!
Jengine ni kwamba kuwezi kumlazimisha mwekezaji kuajiri mtu ambae ahayuko committed na kazi yake hapa kwetu mpaka leo mtu anafanya kazi BAA lkn analalamika anauzishwa pombe na nyie WAWAKILISHI ndio wa mwanzo kulalamika Barazani!..na hakuna utalii bila pombe!
It is very interesting kusikiliza hoja za baadhi ya wawakilishi barazani. Wengi hutoa hoja ambazo zinakinzana na sera za vyama vyao hasa wawakilishi wa CCM. Hii inatokana na kutokujiamini kwao na kutaka kuendelea kuwalaghai wapiga kura wao kwa kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Haiyumkini kwa mwakilishi wa CCM kudai kwamba kero za Muungano hazijatatuliwa bila ya kuorodhesha kero hapo mwanzo zilikuwa ni zipi na ngapi? Wananchi tungependa kujua zilizopatiwa majibu ili tupime uwezo wa serikali ya mapinduzi katika kushghulikia mambo hayo. Hata hivyo, ninachoona mimi ni kuwa baadhi ya wawakilishi walio wengi hawajitumi ipasavyo katika kufanya kazi zao za kuwatumikia wananchi, aidha wamekuwa si watu wa kuchambua taarifa mbalimbali na kuzijengea hoja nzito zenye kuweza kutatua matatizo yaliyopo ambayo kwayo mengi hayana uhusiano na Muungano. Si ajabu kuona mwakilishi akishuhudia kufungwa kwa mjadala wa hoja fulani ilihali hajatenga muda katika siku zote walau kusoma page ya kwanza na mwisho tu. Nyingi ya hoja za barazani hazina mshiko hasa.
ReplyDeleteAidha sikubaliani na hoja iliyotolewa na mwakilishi wa Uzini kwamba kwa Zanzibar kujiunga na OIC kutasaidia uchumi wa Zanzibar. Ni vema Mwakilishi angezama ndani zaidi kuwa kueleza athari zitokanazo na misaada kwa nchi zetu maskini. OIC haipo kwa ajili ya 'charity' na ndiyo maana uanachama wake upo wazi bila ya kuzingatia imani. Ningependa mheshimiwa Raza atafute jopo la wataalam wa uchumi wawe wanapitia hoja zake na kuzijaza uzito ambao utakuwa mchango endelevu barazani. Ni vema tuwaambia wa wawakilishi wetu kuwa bajeti ya matumizi ya Zanzibar itengenezwe kulingana na mapato yanayotarajiwa kupatikana, pili, wawakilishi wasimame barazani wapunguze mishahara, posho na marupurupu mengi ili fedha hizo zitumike katika kuchangia matumizi ya wananchi. Nitaona kuwa wawakilishi wanauchungu sana pale watakapo jileta chini na kujipunguzia wanachovuna kutoka kwenye vijipesa vinavyokamuliwa wananchi walio wengi.
Ni aibu kwa mwakilishi kujisombea rundo la pesa ilhali hospitali ya mnazi mmoja iko hoi bin taaban...au ni kwa sababu haiwahusu? au kwa vile wao hospitali yao ni Muhimbili na Apollo ya India?
Wananchi wasiyumbishwe kwa madai ya Muungano kwani hayo yanaeleweka na yapo katika ratiba ya ufuatiliji katika tume ya pamoja ambayo kwayo baadhi ya wajumbe wa baraza ni wajumbe huko na Makamo wa Pili ni Mwnyekiti Mwenza.
Kana kwamba haitoshi, moja kati ya wizara za SMT yaani ofisi ya makamu Rais inaongozwa na mzazibari na amepewa jukumu la kusimamia Muungano, kwani basi msikae kikao cha pamoja na kupeana taarifa na na jinsi ya utekelezaji?
Ninarudia ni aibu kwa wawakilishi hasa wa CCM kulalamikia haya barazani huku wakijua kuwa wanauwezo mkubwa wa kupata taarifa sahihi ndani wa vyombo vya SMZ na SMT.
Well said ndugu yangu!
ReplyDeleteUnachokisema kiko juu ya mstari, na huo ulaghai ulioutaja tayari umesha jitokeza kwani tokea juzi watu wanamsifia Mh.Raza na Mansour.
Umezungumzia suala la wawakilishi kujituma, ili uweze kujituma ktk mambo kam haya unahitaji pamoja na mambo mengine ELIMU lkn. wengi kati ya wawakilishi wetu hapa hawana elimu stahiki.
Viongozi wetu wanatumia nafasi ya wazanzibari wengi kua na jazba na ushabik dhidi ya muungano ili kujificha kwenye mashina ya njugu .
Hivi inakuwaje SMZ ishindwe kutoa kipao mbele kwa hospitali ya Mnazi mmoja,na kutuacha tukihangaika kwenda kutafuta matibabu Bara ambako nako hali ni ngumu!
Wakati huo huo watu wapo kimya, wanaridhika kwa kuambiwa tu kwamba matatizo yetu yanatokana na muungano lkn mimi nasema, mengi kati ya matatizo yetu yanatokana na sisi wenyewe muungano ni moja tu kati ya matatizo hapa!
Z'bar rushwa imetawala, ufujaji wa mali za umma ktk mashirika ya SMZ, matumizi makubwa ya serikali, ukienda maofisini kazi hazifanyiki, uzembe ndio usiseme, mahakamani ndio kumeoza.
Mimi hua najiuliza hivi inakuaje Mkoa wa DSM una watu zaidi ya 3000000 lkn. una mkuu wa mkoa mmoja Z'bar tuan uwezo gani wa kua wakuu wa mikoa watano? na wote hawa wanalipwa mishahara na posho na kwenye BLW wanaingia! kule hadi baadhi ya bara bara zinajengwa na serikali za mitaa
Kwa kweli sisi tuna mtihani mkubwa lkn viongozi wetu 'wanaenjoy' maana hakuna jambo zuri kama kutawala'dormant society' watu ambao hawana utamaduni wa kuhoji mambo...ushabik mbele tuu!!!