Habari za Punde

Treni ya Zanzibar Bububu Darajani.


Wadau  wangu wengi mamejaribu kuitambua picha hii na wengine kukosa kupatambua mahali hapa ikipita Treni enzi hizo. Wadau wawili wamepatia  sehemu hii  ni  eneo la Saateni katika daraja na ile nyumba inayoonekana ni moja ya nyumba za zamani ikiwa ndani ya JKU.
Nawatakia usiku mwema na mchana mwema wenu mdau. Asanteni kwa kuchangia kutambua eneo hili. Nimeirudia picha hii kutowa jibu sahihi kwa wachangiaji wote waliochangia.

Taasisi husika inabidi kufanya utafiti kuirejesha Treni hii ikiwa inatowa Usafiri kwa kuzunguka Zanzibar kuazia Darajani kupitia Bububu, Bumbwini Mkokotoni.Nungwi, Matemwe Makunduchi na kuishia Darajani ili kutowa fursa ya kurahisisha usafiri na kutembelea sehemu za nje ya mji wa Zanzibar na kuelewa baadhi ya mashamba, kwani kuna watu wengine huishia mjini tu, bila ya kufika maeneo ya mashamba. Changamoto kwa Wizara ya Miundombinu kufaya utafiti huo kama inawezekana.      

1 comment:

  1. Safi sana mkuu!
    Ila ukibahatika kupata nyengine usiache kuturushia, zinatupa changamoto za maendeleo na kutukumbusha zamani.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.