Habari za Punde

Mlinzi kampuni ya uwindaji ajeruhi kwa riasi

Joseph Ngilisho, ARUSHA
KAMPUNI ya uwindaji ya Mwiba holdings ya jijini Arusha inayomilikiwa na wakili maarufu nchini, Nyaga Mawala imeingia kwenye kashfa baada ya askari wake kummiminia risasi na kumjeruhi vibaya mfugaji  ambaye amelazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi(ICU) wilayani Arumeru.

Mfugaji huyo ametambulika kwa Kitabungéta Kitajuri (25)mkazi wa kijiji cha Kakesyu, Endulen wilaya ya Ngorongoro alinusurika kufa baada ya askari wa kampuni ya uwindaji  ya Mwiba ya jijini Arusha, kumjeruhi kwa risasi wakati akitafuta mifugo yake iliyokuwa imepotea.

Akizungumza kwa tabu katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) katika hospitali ya Selian alipolazwa, Kitajuri alisema kuwa tukio hilo lilitokea julai 8 mwaka huu majira ya saa 8 mchana baada ya askari hao kumkuta kandokando ya eneo la uwindaji.

Kwa mujibu wa Kitajuri, askari  hao wa wanyama pori walikuwa watatu kwenye gari la wazi aina ya Landrover na  kwamba baada ya kumwona walisimamisha gari na mmoja wa askari hao alimfyatuli risasi za kutosha na kumjeruhi vibaya sanjali na kumvunja mkono wa kushoto.

"Hao askari walikuwa watatu kwenye gari walioniona walisimamisha gari bila hata ya kuniuliza walianza kunifyatulia risasi na baada ya kuona nimeanguka chini waliwasha gari na kuondoka kwa mwendo mkali’’alisema Kitajuli

Alifafanua kuwa siku ya tukio majira ya mchana alipoteza ng’ombe wake 10 na kuhisi kwamba pengine watakuwa wamekimbilia kwenye chemchem ya maji iliyopo kando kando na eneo la uwindaji la wakili Mawala, ambapo alipokaribia ndipo alipokutana na askari hao.
Akizungumzia tukio hilo shemeji yake aliyejitambulisha kwa jina la Shegwega Kidamani ambaye anamuunguza alisema kuwa walipata taarifa kutoka kwa wasamalia wema kuwa ndugu yake huyo alikuwa amepatwa mkasa wa kupigwa  risasi na askari wa wanyama pori na kwamba alikuwa na hai mbaya.

Alisema walijaribu kufuatilia na kumkuta amelala kwenye majani bila msaada wowote damu nyingi zikivuja,ndipo waipoamua kumpeleka hospitali ya Enduleni iliyopo wilayani humo.

Kwa mujibu wa daktari waliokuwa wakimtibu hopitalini hapo ambaye aligoma kutaja jina lake akidai si msemeji, alisema kuwa hali ya mfugaji huyo bado ni mbaya na kwamba bado yupo kwenye uangalizi wa hali ya juu na jitihada za kuondoa risasi zilizokuwa mwili mwae walikuwa  bado wanaendelea.

Kampuni ya Mwiba Holding ipo mpakani mwa mkoa wa shinyanga katika wilaya ya Maswa na kwamba mara nyingi kampuni hiyo imekuwa ikikumbwa na matukio ya kupiga risasi wananchi wanaoishi eneo hilo na maiti zao zimekuwa zikiokotwa bila kujua ameuawa lini.

Jitihada za kumpata mmiliki wa kampuni hiyo Nyaga Mawala zilishindikana baada ya kutopokea simu licha ya kutafutwa mara kadhaa kupitia simu yake ya mkononi ,ambapo simu ilikuwa ikiita bila kupokelewa hata alipotumiwa ujumbe wa simu hakuweza kutoa ushirikiano.

Kwa upande wa kamanda wa polisi mkoani Arusha,Liberatus Sabas alipoulizwa alisema kuwa alikuwa bado hajapata taarifa na kuahidai kuzifuatilia.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.