Mahmoua Ahmad, ARUSHA
KAMATI ya kudumu ya Bunge ya maendeleo ya jamiii imeitaka serikali kuharakisha muswada wa habari mapema ili uweze kupelekwa bungeni na kujadiliwa kwa lengo la kutatua changamoto mbalimbali ambazo zinaikumba sekta ya habari nchini.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Juma Nkamia alitoa tamko hilo kwa niaba ya kamati nzima juzi mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea kituo cha radio cha radio 5 fm kilichopo Njiro nje kidogo la jiji la Arusha.
Akizungumza mara baada ya kuhitimisha ziara hiyo, Nkamia alisema kwamba ni muda sasa serikali inatakiwa kuharakisha kuuleta muswada huo bung ili uweze kujadiliwa na kupitishwa kwa lengo la kuokoa sekta ya habari nchini.
"Nadhani sasa ni muda wa serikali kuharakisha mapema waulete huu muswada wa habari ili wabunge tuweze kuujadila na kuupitisha kuokoa hii sekta ya habari nchini", alisema Nkamia
Alisema kwamba sekta ya habari nchini imekuwa ikikabiliwa na chanagamoto lukuki kama tatizo la waandishi kutokuwa na weledi na maadili mema hivyo muswada huo utasaidia kuwabana waandishi hao ambao wamebatizwa jina la "makanjanja".
Hatahivyo,aliutaka uonmgozi wa radio hiyo kujikita kuhakikisha kwamba wanaandaa vipindi vingi vya vijijini kwa lengo la kuwapa sauti watu wa maeneo hayo hususani wanawake na wakulima.
Awali akitoa risala yake mbele ya kamati hiyo,mkurugenzi wa radio hiyo,Robert Francis alisema kwamba wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali hususani katika maeneo ya utendaji kazi kama suala la mfumo wa digitali.
Alisema kwamba ni muda wa kamati hiyo kuzishauri halmashauri mbalimbali nchini kuzipatia matangazo radio zilizopo ndani ya halmashauri hizo kwa lengo la kuongeza kipato na kuzifanya radio hizo ziweze kujiendesha.
Alisema kwamba mikakati ya kituo chao ni kufungua chuo cha uandishi wa habari kitakachosaidia kuwanoa waandishi mbalimbali waliopo ndani na nje kituo hicho pamoja na kufungua kituo cha runinga kitakachokuwa cha kwanza kurusha matangazo yake mkoani Arusha.
No comments:
Post a Comment