Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Anne Makinda,akiongoza Ujumbe wa Wabunge hilo walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kutoa pole kwa Rais,kutokana na msiba wa ajali ya Meli ya Mv Skagit ya Kampuni ya Segul iliyozana juzi Ikitokea Dar es Salam na kuelekea Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Anne Makinda,akiongoza Ujumbe wa Wabunge hilo walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kutoa pole kwa Rais,kutokana na msiba wa ajali ya Meli ya Mv Skagit ya Kampuni ya Segul iliyozana juzi Ikitokea Dar es Salam na kuelekea Zanzibar
dah huyu mama ana roho ngumu kweli anakuja kufanya nini kama alishindwa kuwapa rohusa wabunge wetu mpaka waziri kaingilia kama bora kwa usalama wake alivyo kwenda ikulu lakini angekuja mitaa ingekuwa balaa
ReplyDeleteMisaada ya fedha intolewa lakini bado kuna wale wa maafa ya mwaka jana ambao bado hawafikiriwa chochote,nasikia pia balozi seif kanunuwa bonge la nymba sehemu fulani,nyumba ilijengwa na mzenj aloko nje ya nchi ambae ameamuwa kuiyuza bada ya mauza uza ya huko nyumbani
ReplyDeleteW'bari wakati umefika kujenga utamaduni wa kutatua matatizo yetu badala ya kuyahamishia kwa wengine.
ReplyDeleteMimi bado sijaliona kosa kubwa alilo lifanya spika wa Bunge kwa kuwataka Wabunge wa Z'bar kusubiri ili utaratibu wa kibunge kuja Z'bar uandaliwe.
Hata hao wabunge waliokurupuka na kujifanya wana uchungu sijuona huo msaada mkubwa walioutoa, ni jazba tu na hii ndio iliyoifikisha Z'bar hapa ilipo.
Wabunge na wawakilishi wetu kama kweli wanaipenda Z'bar wanashindwa nini kuishauri SMZ kuweka kituo cha KMKM chenye boti na mawasiliano ya redio pale NUNGWI ilikufatilia mienendo ya vyombo vinavyosafiri baina ya Pemba na Uguja pamoja na kuweka kituo kama hicho pale PUNGUME au CHUMBE ili kufuatilia vyombo vinavyo safiri baina ya Z'bar na Bara?
Lazma tukubali sisi bahari ndio mmaisha yetu na hatuwezi kuikwepa, ndugu zangu wakati umefika kuacha uvivu wa kufikiri na kuiwacha KMKM kukusanya boti pale KIBWENI huku maafa yanatokea.
Mwisho nawaomba ndugu zangu tuwache JAZBA na utamaduni wa PROBLEM TRANSFER hautatufikisha popote, bali kubwa zaidi utatujengea uhasama na chuki kwa watu ambao hatuwezi kuwaepuka kutokana na ukaribu wetu kijografia!