RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amemteua Dk. Mohammed Hafidh Khalfan kuwa mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mafunzo ya Amali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, ilieleza kuwa Dk. Shein amefanya uteuzi huo chini ya kifungu 9(1)(a) cha sheria nambari 8 ya Mafunzo ya Amali Zanzibar.
Dk. Abdulhamid alisema uteuzi wa Mwenyekiti huyo umeanza rasmi Juni 30 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment