Habari za Punde

Tunzo za Zanzibar Music Award Salama Bwawani Zanzibar.

Msaani wa Muziki wa Zenj Flava Baby Jay akiwatowa burudani katika Tamasha la Tunzo ya Zanzibar Music Award iliofanyika Salama Bwawani Hoteli.
Makamu wa Rais wa Tanzania Dk.Mohammed Gharib Bilal. akimkabidhi Tunzo Msani wa Mwaka 2011 Bi Mwanacha Hassan, kwa kuwa msani wa mwaka, utoaji wa Tunzo hizo umefanyika ukumbi wa Salama Bwawani na kushoto Mkurugenzi Biashara wa Kampuni ya Simu ya ZANTEL Mohammed Mussa. 
Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal akiwa katika picha ya pamoja na  Waandaaji wa Tunzo hiyo ya Zanzibar Music Award, baada ya kutowa Tunzo ya Mwaka kwa Msanii Bora Zanzibar Bi Mwanacha Hassan..
Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal , akitowa nasaha zake kwa Wananchi na Wasanii mbalimbali waliohughudhuria Tamasha la kutowa Tunzo kwa Wasanii Bora kwa Mwaka 2011, lililofanyika ukumbi wa salama bwawani.
Kaka Abuubakari Liongo ndani ya nyumba akishuhudia utoaji wa Tunzo za Wasanii Bora kwa mwaka 2011. akiwa na heti kubwa na kupozi kati siti yake bila ya bughudha. akiwa na wadau wengine
Wapenzi wa Muziki  katika iwa vya Zanzibar wakishuhudia utoaji wa Tunzo kwa Wasanii Bora wa Mwaka 2011 katika Ukumbi wa Salama Bwawani.
Masharubaro wakiwa na Msanii wao baada ya kupokea Tunzo yake.

Mkurugenzi wa Zanzibar Media Corporation  Mhe.Mohammed Seif Khatib, akitowa machache kuhusu  utoaji wa Tunzo kwa Wanamuziki Bora wa Mwaka 2011  uliofanyika ukumbi wa salama bwawani.
Meneja Matangazo wa Kampuni ya Scanad Obeni Swai, akitowa Tunzo kwa Msanii bora
Mkurugenzi wa Zanzibar Media Corporation  Mhe Mohammed Seif Khatib, akimkabidhi Tunzo ya Muimbaji Bora wa Taarab Asilia Rukia Ramadhani.
Baby Jay akitowa shukrani kwa wapenzi wake kwa kumuezesha kutowa Tunzo ya Msanii Bora wa Kike Muziki wa Kiksasa.









Afande Sele akitowa burudani katika Tamasha la kutowa Tunzo kwa Wasanii Bora wa 2011 liliondaliwa na ZMC na  kudhaminiwa na kampuni ya simu ya Zantel.

1 comment:

  1. Kaka hapa umetunyima raha ya maelezo ktk picha. Huyu aliesimama na Mh. Seif anaonekana kama Bi Rukia Ramadhani sijui ndie?

    Mambo kama haya yanatukumbusha zama zile za taarab rasmi kataka miaka ya 80!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.