Habari za Punde

Uvuvi haramu waendelea Menai


Na Madina Issa
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Abdilah Jihad Hassan amesikitishwa na kitendo alichokishuhudia cha ukiukwaji mkubwa na taratibu za uvuvi katika bahari ya ghuba ya Menai.

Waziri huyo alibaini hayo alipokuwa katika ziara ya hafla ya kukagua shughuli za uvuvi katika bahari ya Kizimkazi, moja ya vijiji vinavyounda ghuba ya Menai.

Waziri huyo alishuhudia baadhi ya wavuvi wakitega nyavu zilizokuwa sio halali kwani inapelekea hata samaki kutopatikana katika bahari hizo.

Aidha alibaini ukiukwaji mkubwa wa taratibu za uvuvi kwani inafanya hata kupotea kwa samaki ambao ndio wakubwa na wenye kiwango.

Hata hivyo alisema kuwa haitokuwa busara kwa wavuvi kuendelea na uvuvi huo kwani itapelekea hata kupotea kwa samaki ambao wananchi mbalimbali wamekuwa wanawahitaji kiasi kikubwa.

"Hali niliyoikuta nilipokuwa baharini kwa kweli sio hali ya kawaida hivyo hatuna budi kuwachana na uvuvi huo ambao hauna tija kwa taifa letu na hata vizazi vyetu", alisema Jihadi.

Hata hivyo aliwataka wavuvi kuwa na mashirikiano ya hali ya juu na pia kuzifuata sheria zilizowekwa na wao wenyewe kuwataka washirikiane na wizara hiyo hata hivyo wajiepushe na tabia waliokuwa wanayo hivi sasa kwani itapelekea kufanya ugomvi kwa wavuvi na wanakijiji.

Hata hivyo wavuvi wanaoshuhulikia uvuvi huo waliokutikanwa wakiendelea na uvuvi huo haramu walisema wataendelea na uvuvi huo na hawatouwacha kwani uvuvi huo ndio unaowapa tija na kula yao ya kila siku.





No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.