Mwashungi Tahir na Salama Thalaba (ZJMMC)
WAKAAZI wa mji Mkongwe wamelalamikia kuwepo uvunjaji wa maadili unaoyofanywa na vijana katika eneo la bustani ya Wananchi 'Jamhuri garden' ambayo inayosababisha muonekano wa taswira mbaya katika jamii na wageni kwa ujumla.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti wakaazi wa maeneo jirani na bustani hiyo,walisema kuwa busatani hiyo imekuwa ikitumika vibaya kinyume na inavyotakiwa jambo ambalo limekuwa likichochea vishawishi vya kila aina hasa kwa vijana ambao ndio watunmiaji wakubwa wa bustani hiyo.
Ali Mohammed miongoni mwa wakaazi wa mji mkongwe alisema kuwa, baadhi ya watu wamekuwa wakiitumia bustani hiyo kwa mambo ya kimapenzi jambo ambalo linaharibu taaswira nzima ya bustani hiyo.
"Tunawaomba wahusika wa hii busatni kuliangalia kwa kina hili kwani ni njia moja ya kuharibu watoto wetu, hivyo tunataka wachukuliwe hatua za kisheria," alisema.
Aidha alisema wengi wanaotumia bustani hiyo ni vijana ambao ni wanfunzi, ambapo hujishirikisha katika vitendo viovu.
Nae Suzan Christopher, alisema Anashangazwa na vitendo vinavyofanyika bustanini hapo, kwa kuwa wamekuwa wakitumia bustani hiyo kwa mambo yasiofaa.
Kwa upande wake mkuu wa bustani wa Baraza la Manispaa, Maulid Abdullah Hassan, amethibitisha kuwepo kwa vitendo hivyo na kuitaka serikali kuwaongezea ulinzi katika sehemu hiyo ili kuepisha vitendo hivyo.
Alisema vijana wengi hawajui lengo la bustani na kwamba hutumia sehemu hiyo kama starehe kinyume na ilivyotarajiwa.
Vile vile alisema lengo la bustani ni kupamba mji na kuuweka vizuri mandhari na haiba ya mji zanzibar uzidi kuvutia ikiwa kwa wageni na wazanzibar wenyewe.
Hata hivyo, aliitaka jamii kufatilia nyendo za watoto wao kwa kuwa baadhi yao wamekuwa wakitoroka majumbani mwao na kufanya vitendo viovu katika bustani hiyo.
No comments:
Post a Comment