Na Mwajuma Juma
ZAIDI ya shilingi milioni 100 zinatarajiwa kutumika katika matengezo ya uwanja wa Mao Dze dong yanayoendelea hivi sasa.
Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki, Mjumbe wa kamati tendaji ya Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) Hafidh Ali Tahir, ametaja miongoni mwa maeneo yaliyopewa umuhimu katika matengenezo hayo, ni sehemu ya kuchezea ‘pitch’, uchimbaji wa kisima ambao unagharamiwa na chama hicho.
Alieleza kuwa, ZFA imeamua kuutengeneza uwanja huo ili Zanzibar ipate eneo zuri la kufanyia mashindano yake ya soka ikiwemo ligi kuu inayotarajiwa kuanza Septemba 8, mwaka huu.
“Kama mnavyojua, miongoni mwa mambo yanayoifanya ligi yetu ikose mvuto na adha, ni ubovu wa uwanja wa Mao, sasa tumeamua kuufanyia matengenezo kwa kuuburuga wote ili tupande majani upya, na kuupa sura nzuri”, alifafanua Tahir.
Kwa kuanzia, Tahir alisema sehemu ya kuchezea ‘pitch’ pamoja na uchimbaji wa kisima ndiyo mambo ya kwanza, na baadae wataangalia maeneo mengine, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vyoo.
Hata hivyo, alisema kiasi hicho cha fedha huenda kikaongezeka
maradufu, ikizingatiwa matengenezo hayo yameanza bila kufanyiwa tathmini, bali yanafanywa kwa mujibu wa mahitaji yanavyoelekezwa.
maradufu, ikizingatiwa matengenezo hayo yameanza bila kufanyiwa tathmini, bali yanafanywa kwa mujibu wa mahitaji yanavyoelekezwa.
Mao Dzedong ni uwanja mkongwe hapa Zanzibar na Afrika Mashariki ulijengwa na Jamhuri ya China miaka ya mwishoni mwa 40, ambao uliwahi kuchezewa mashindano ya Gossage (sasa Challenge), lakini kwa miaka mingi umekabiliwa na uchakavu ikiwemo kuanguka kuta zake.
>Mao Dzedong ni uwanja mkongwe hapa Zanzibar
ReplyDelete>na Afrika Mashariki ulijengwa na Jamhuri ya >China miaka ya mwishoni mwa 40,
Jamani hii sio kweli. Huu uwanja haukuitwa Mao Dse Tung kwasababu ulijengwa na China.
Mwajuma hapo umefurunda!