Habari za Punde

Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM yakutana Zanzibar


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi wa CCM,alipowasilikatika viwanja vya Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar,kushiriki katika kikao cha siku moja cha Kamati maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ya Zanzibar,kilichofanyika leo.
Makamo Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk.Amani Abeid Karume, akiendesha kikao cha kamati maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ya Zanzibar,katika ukumbi wa CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar,(kushoto) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Dk.Ali Mohamed Shein


Wajumbe wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar,wakiwa katika kikao cha siku moja chini ya Mwenyekiti wake, Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk.Amani Abeid Karume,wakiwa katika ukumbi wa CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar,kilipofanyika kikao hicho leo. [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

3 comments:

  1. majambazi yanakutana kuuhami muungano , hakuna jengine bali ni kutafuta njia za kutafuta kuendeleza ukoloni na dhulma kutoka kwa watanganyika, wamevaa vikofia na vihijabu kama vile wanamuogopa Mungu kweli , kumbe wamejaa chuki na dhuluma , mwenyezi Mungu atakilaani kikao chenu hicho , na nyinyi mliopo kwenye picha mtakutana na Mola wenu kujibu masuala mazito , ibada zenu hazitosaidia , kwa kuwa Munga ameshatangaza hawapendi wenye kudhulumu

    ReplyDelete
  2. Allah ndiye mjuzi wa yote kama kikao chao ni kibaya inshaallah Allah atatulinda na atatuhifadhi na kama kikao hicho ni cha wema Allah atawaongoza na kukipa nguvu kikao chao. Amin inshaallah.

    ReplyDelete
  3. dalili ya mvua ni mawingu nd JK ,usitegemee zuri lolote kwenye kikao hicho zaidi ya kupanga jinsi ya kuwahujumu wananchi wa znz kwa kutumia polisi na majeshi yaliyolaaniwa na Mungu Mtukufu na hakika adhabu kali isiyo kifani itawaangukia wote wenye nia mbaya na waznz na iada zao zote na kufuturisha watatiliwa vikapuni na Mola watupiwe usoni , tunakuomba mola utukubalie dua yetu muungano huu uwe ni kitandawili na kitu kilichopitwa ,

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.