Habari za Punde

Balozi Seif aendelea na ziara yake kukagua vitengo vya afya

 Daktarimstaafu wa Huduma za Macho anayejitolea katika Hoaspitali ya Jimbo la  Kwamtipura iliyopo Mikunguni Dr. Ashraq JumaHaji akielezea changamoto anazopambana nazo katika kazi zake mbele ya Makamu waPili wa Rais wa ZanzibarBalozi Seif Ali Iddi aliyefanya ziara ya kukagua shughuli za hospitali hiyo. ulia ya Dr. Ashraq ni KatibuMkuu wa Wizara ya Afya Dr. Saleh Mohammed Jidawi
 Makamu waPili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimpa pole Mtoto  Nafdat Mwalimu Kheir aliyelazwa katikaHospitali ya Makunduchi baada ya kuungua maji ya Moto Ijumaa iliyopita.
 Makamu waPili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja naUongozi wa Hospitali ya Wilala ya kusini iliyopo Makunduchi. ushoto yake ni Meneja waHaospitali hiyo Dr. Zainab Mohd na kulia ya Balozi ni Katibu Mkuu wa Wizaraya  Afya Dr. Saleh Mohammed Jidawi naKatibu wa Hospitali ya Makunduchi Bwana Mgana Othman Mgana.
 Makamu waPili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja njaWafanyakazi wa Hospitali ya Mikunguni, Viongozi na Wananchi walioshiriki nakusimamia ujenzi wa Hospitali hiyo ya Jimbo la kwamtipura.

 Mkuu waKituo cha Afya cha Jambiani Dr. Hamza Mwalimu Omar akizungumza na Makamu wa Piliwa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akikitembelea kituo hicho ndani ya ziara yake katika Taasisi zilizomo ndani ya Wizara ya Afya.

Na Othman Khamis Ame

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema pamoja na jitihada zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali za uimarishaji wa Sekta yaAfya lakini bado Wananchi wana wajibu wa kuchangia baadhi ya huduma katikaSekta hiyo muhimu kwa Jamii.
 
Balozi Seif lisema hayo wakati akiendelea na awamu ya pili ya Ziara yake katika Taasisi zilizomo ndani ya Wizara ya Afya Zanzibar ikiwa ni mwanzo wa mpango wake wa kuzitembelea Wizara za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 
Balozi Seif ambaye alipata fursa ya kuzitembelea Hospitali za Jimbo la Kwamtipura iliyopo Mikunguni, Kituo cha Afya cha Fuoni , Kituo cha Afya cha Jambiani pamoja na Hospitali ya Wilaya ya Kusini iliyopo Makunduchi alisema nia ya Serikali ni kusambaza Huduma za Afya katika maeneo yote ya Jamii Mjini na Vijijini bila ya Malipo.

Hata hivyo alisema katika kuunga mkono juhudi hizoWananchi wana paswa kuchangia baadhi ya huduma katika Vituo na hospitali za Serikali hasa pale inapohitajika kufanya hivyo kwa lengo la kuimarishaupatikanaji wa huduma hizo.
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameuomba Uongozi wa Wizara ya Afya Zanzibar kuangalia uwezekano wa kuitumia Hospitali ya Kwamtipura kama Tawi la Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja katika baadhi ya Vitengo vyake.
 
Balozi Seif alisema Hospitali hiyo ingawa imejengwa kwa ajili ya kutoa huduma za afya kwa wakaazi wa Jimbo la Kwamtipura na maeneo ya jirani lakini bado inaonekana kuwa na nafasi kubwa nay a kutosha ya kutumiwa ikiwemo pia kulazwa wagonjwa.
 
“ Nimefurahi kuona huduma nzuri zinazotolewa naHospitali hii. Lakini pia zipo fursa nyingi ambazo hazijatumiwa ndani ya Hospitalihii. Kwa nini Uongozi wa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja wasiitumie fursa hizizilizopo?”. Alishauri Balozi Seif.
 
Amewapongeza Madaktari, Wauguzi na Wafanyakazi  wote wa Hospitali na Vituo vya Afya vyaKwamtipura, Fuoni, Jambiani  naMakunduchi kwa jitihada zao za kuwapatia huduma bora Wananchi.
 
Balozi Seif aliwahakikishai watendaji hao wa Sekta ya Afya kwamba Serikali kwa kushirikiana na Wizara ya Afya watasaidiana katika kuzipatia ufumbuzi changamoto na kero zinazowakabili watendaji hao katika sehemu zao za kazi.
 
“ Serikali itajitahidi kuona utendaji wenu unaimarika vyema lakini hilo ni vyema likaenda sambamba pia na nyinyi kujitahidi kufanya kazi zaidi”.Alisisitiza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
 
Akizungumzia suala la Uzio kwa Hospitali ya Wilaya kusini huko Makunduchi Balozi Seif aliushauri Uongozi wa Hospitali hiyo kutafuta mbinu za kuzunguusha uzio hata kama utakuwa wa muda.
 
Alisema hatua hiyo itaweza kusaidia ulinzi wa eneo hilo vyenginevyo tatizo la uvamizi katika eneo hilo litashindwa kuzuilika.
 
Kwa upande wao baadhi ya waratibu na wakuu wa Vituohivyo vya Afya walimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba lipotatizo la uhaba wa wafanyakazi wa kudumu kwa baadhi ya vituo na Hospitali hizojambo ambalo linapunguza kasi ya uwajibikaji wao.
 
Walitoa mfano wa Mfanyakazi wa baadhi ya Vitengo kama Meno kufanya kazi katika vituo viwili vya Afya hali inayopelekea kituo kimojakwa siku hiyo kukosa huduma  hizo muhimu.
 
Hata hivyo Wakuu hao wa Vituo vya Afya na Hospitali walifahamisha kwamba yapo mafanikio makubwa ya uimarikaji wa huduma za afya za Wananchi kutokana na elimu kubwa inayoendelea kutolewa katika vituo hivyo hasasuala la ushauri nasaha na Uzazi wa Mpango na salama.
 
Mapema Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dr. Saleh Mohammed Jidawi alisema uimarishaji wa huduma za afya ya msingi katika maeneo ya Wananchi ndio unaopelekea kupata Jamii yenye afya na nguvu za uhakika.
 
Dr. Jidawi alisema Zanzibar imefanikiwa kuwa na miundo mbinu mizuri ya huduma za Afya inayotokana na kuwana Vituo vingi vya Afya vinavyokadiriwa kufikia 140 Unguja na Pemba.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.