JUMUIA
ya watu wenye ulemavu Wilaya ya Micheweni
Mkoa wa Kaskazini Pemba,
wameiomba Serikali na taasisi binafsi kuwapatia ruzuku kwa ajili ya kuendeleza jumuia yao .
Hayo yalielezwa na Mwenyekiti wa Jumuia
hio Ali Mussa Khamisi, huko Ofisini kwake Micheweni wakati alipokua akizungumza
na mwandishi wa habari wa habari hii juu ya suala hilo .
Alisema kuwa serikali haina budi
kushughulikia jumuia hio kwa kuwapatia ruzuku kwa lengo la kuendeleza jumuia
hio kwa kuwaenua kimaslahi zaidi na kuepukana na usumbufu unao wapata kwenye
jumuia yao .
Alieleza kuwa kutokana na hali ngumu ya
kimaendeleo na hali za walemavu hao wanashindwa kutekeleza baadhi ya shughuli
muhimu kulinganisha na uhaba wa kifedha na kukosa mitaji ya kundesha jumuia yao .
Aidha alisema kuna baadhi ya watu wasio
na ulemavu kuendelea kuwanyanyapaa wanaishi na ulemavu na kuwaona kama hawana haki ya kushiriki katika shughuli zozote za
kimaendeleo jambo linalowanyima fursa walemavu wilayani humo.
Alifahamisha kuwa suala la
kunyanyapaliwa kwa walemavu hao linakuwa likionekana hata katika Nyanja za
uongozi kutokana na ulemavu unaowakabili wanajumuia hao.
Hata hivyo aliitaka jamii kutokuwabagua
watu wanaoishi na ulemavu na kuwaona kama
wengine kwani ulemavu sio kifo na badala yake kuwanasihi kushirikiana
kikamilifu katika shughuli mbali mbali za kimaendeleo.
Kwa
upande wake mmoja kati ya wanachama wa jumuia hio Sharifa Faki Mwana
alisema ipo haja kuwaona walemavu kwani tangu kuanzishwa kwa jumuia hio hakuna
kitu chochote walichofaidika nacho.
“Hatuna tulicho nufaika nacho tokea
kuanzishwa kwa jumuia hii kwa ajiliya kutusaidia japo katika shughuli ndogo
ndogo za kutuwezesha katika jumuia”,Alisema mwanachama huyo.
Alisema jambo zuri zaidi ni mashirikiano baina ya viongozi
wa jumuia,Serikali na hata makampuni binafsi kuwasaidia ili waweze kujikwamua
kimaisha na kuondokana na kuonekana kama ni watu wanaopenda kuombaomba wakati
wote.
“Sisi
watu tunaoishi na ulemavu maisha yetu tunaonekana kama
ni watu wa kuhangaika na kuombaomba watu jambo ambalo linatukatisha tama ya
kimaendeleo”,alilalama mwanachama huyo.
Sambamba na hayo aliwataka viongozi wa ngazi
mbalimbali kuelekeza nguvu zao kwa lengo la kuondokana na kadhia pamoja na aibu
zinazoendelea kuwakumba walemavu.
Jumuiya ya watu wenye ulemavu Wilaya ya
Micheweni Mkoa wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, ilianzishwa mwaka 1985 na ilianza na
wanachama 150 kama waanzilishi na hadi kufikia leo hii inawanachama 706 ndani
ya jumuia hio.
No comments:
Post a Comment