Na Mwandishi Maalum UAE
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif
Sharif Hamad amekutana na uongozi wa shirika la misaada la mwezi mwekundu
kuzungumzia masuala mbali mbali yakiwemo ya kuipatia misaada
Zanzibar.
Viongozi hao ambao wamekutana mjini
Abudhabi katika falme za nchi za kiarabu UAE, wameahidi kuendeleza ushirikiano
na uhusiano wa muda mrefu uliopo kati ya Zanzibar na UAE.
Katibu Mkuu wa shirika hilo Dr. Mohd
Ateeq Al Falahi, amemuahidi Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kuwa Shirika
hilo la kimataifa la Red Crescent, litaendeleza misaada yake kwa Zanzibar na
nchi nyengine duniani.
Shirika hilo limekuwa
likijishughulisha na utoaji wa misaada kwa nchi mbali mbali dunia ikiwemo
misaada katika sekta za elimu na afya.
Makamu wa Kwanza wa Rais anatarajiwa
kurejea nchini kesho baada ya kumaliza ziara yake ya wiki mbili nchini Marekani
na Uingereza.
No comments:
Post a Comment