Habari za Punde

Mawaziri wa Katiba na Sheria wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar na Serekali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Watembelea Ofisi za Tume ya Katiba.

NaMwandishi Wetu, Dar es Salaam
Tume ya Mabadiliko ya Katibaimesema imejipanga kukamilisha majukumu ndani ya muda uliowekwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 nahivyo nchi kuwa na Katiba Mpya ifikapo mwezi Aprili, 2014.
Mwenyekiti wa Tume hiyo JajiMstaafu Joseph Warioba amewaeleza Mawaziri wa Katiba na Sheria kutoka Serikaliya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwapamoja na changamoto zilizopo, dhamira hiyo ya Tume ipo palepale.
Mawaziri hao, Bw. MathiasChikawe wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Bw. Abubakar Khamis Bakari wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibarwalitembelea ofisi za Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (Jumatatu, Septemba 3,2012) ili kujionea utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Tume hiyo.
“Tunafahamu hii nichangamoto, lakini tumeikubali na tutajitahidi kufanya kila liwezekanalokuhakikisha kama Taifa tunakuwa na Katiba Mpya ifikapo tarehe 26 Aprili, 2014,”alisema Jaji Warioba  katika mkutanoMawaziri hao ambao walitembelea vitengo vya Utafiti na Taarifa Rasmi (Hansard).
Jaji Warioba amesema kuwalengo hilo la Tume linaongozwa na sababu kuu mbili ambazo ni Sheria yaMabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ambayo inaipa Tume muda wa miezi 18 kutekelezamajukumu yake. Tume hiyo ilianza kazi mwezi Mei mwaka huu (2012).

Kwa mujibu wa Jaji Warioba,sababu ya pili ni hali ya kisiasa ilivyo hapa nchini ambayo amesema Taifalinahitaji kuwa na mwafaka wa kisiasa kupitia Katiba kabla ya mwaka 2015.
“Ukiangalia hali ya kisiasa,tunadhani itakuwa vizuri tukiwa na Katiba Mpya kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015,”alisema Jaji Warioba katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na Naibu Waziri waKatiba na Sheria Bi. Angellah Kairuki, Katibu wa Tume Bw. Assaa Rashid na NaibuKatibu wa Tume Bw. Casmir Kyuki.
Pamoja na nia hiyo, JajiWarioba pia aliwaeleza Mawaziri hao kuwa kwa sasa Tume yake imejikita katikakukusanya maoni binafsi ya wananchi na kuwa baada ya hatua hii, Tume itaanzakukusanya maoni ya makundi mbalimbali kama vyama vya siasa, taasisi za kidini,jumuiya za kitaaluma na asasi za kiraia.
Akizungumza katika mkutanohuo, Waziri wa Katiba na Sheria Bw. Mathias Chikawe alieleza kufurahishwa nautekelezaji wa majukumu ya Tume na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kutoaushirikiano kwa Tume ili kuhakikisha malengo yake yanafikiwa.
“Kwa niaba ya Serikalinapenda nikuhakikishia tena kuwa tutaendelea kuwapa kila aina ya ushirikianomtakaouhitaji ili mtekeleze majukumu yenu kwa ufanisi,” alisema Waziri Chikawe.
Kwa upande wake, Waziri waKatiba na Sheria wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Abubakar Khamis Bakari aliwapongeza watendaji waSekretarieti hiyo kwa ubunifu 
“Huu mfumo wa teknolojia wa kupokea na kuyafanyia kazi maoni yawananchi ni mzuri na ingekuwa umetengenezwa na mtaalam kutoka nje, ingekuwagharama kubwa,” alisema Waziri huyo  wakatiakizungumzia mfumo wa kompyuta ulitengenezwa na wataalam wa Teknolojia yaHabari na Mawasiliano (TEHAMA) wa Tume hiyo.
Tume ya Mabadiliko ya Katiba hivi sasa inaendelea na kazi ya kukusanyamaoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya kupitia mikutano katika mikoa saba yaMorogoro, Lindi, Katavi, Kigoma, Mwanza, Mbeya na Ruvuma. Tayari Tume hiyoimeshakusanya maoni katika mikoa ya Tanga, Manyara, Kagera, Shinyanga, Dodoma, Pwani,Kusini Unguja na Kusini Pemba.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.